Helkopta ya polisi pamoja na gari vikiwa eneo la mapango ya Amboni, Tanga wakati wa mapambano ya polisi na kundi linalodhaniwa kuwa la kigaidi |
.
Wanausalama wakiwa eneo la mapango ya Amboni, Tanga kupambana na kikundi kinachodhaniwa kuwa cha kikaidi.
WADAU naomba sasa niwape ukweli wa kinachojiri Tanga kuhusu sakata la kigaidi.
Wiki moja, polisi walimkamata mtuhumiwa mmoja anayejulikana kwa jina la Master ambaye inasemekana ndiye aliyekuwa akiratibu uporaji wa silaha kwenye vituo vya polisi na polisi wenyewe.
Matukio haya yametokea kule Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani baada ya kituo kuvamiwa na Tanga, Chumbageni kwa askari kuporwa silaha wakiwa katika doria.
Katika kutumia weledi wao wa kupata habari, ililazimika sasa polisi waende eneo ambalo mtuhumiwa anasema ndiko silaha wanazopora zilipofichwa.
Alieleza silaha wanaficha maeneo ya Amboni ambako Wachina waliojenga barabara ya Horohoro waliweka kambi.
Kwa hiyo magaidi hayo hayapo mapango ya Amboni tunayoyafahamu.
Baada ya kufika eneo la tukio mtuhumiwa akiwa na pingu alijirusha kwenye pango hilo huku polisi wakiwa wanashangaa nini kimetokea.
Baada ya kufika eneo la tukio mtuhumiwa akiwa na pingu alijirusha kwenye pango hilo huku polisi wakiwa wanashangaa nini kimetokea.
Ikumbukwe mtuhumiwa huyo alikuwa na pingu. Baada ya mtuhumiwa tu kutua chini au kiliposikika kishindo basi haikupita muda mvua ya risasi ilianza kunyesha kuelekea polisi walipo pamoja na mabomu ya kurusha kwa mikono.
Bomu mojawapo lilifanikiwa kumjeruhi askari polisi mmoja ambaye ameshonwa nyuzi kama kumi na moja hivi.
Baada ya kuona hali imekuwa ngumu ilibidi OCD aliyekwenda kwenye tukio kuomba msaada zaidi kwa FFU, Tanga. Napo hali ikawa tete, ndipo ilipolazimu kuomba msaada kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Kama uelewevyo kuomba Jeshi la Wananchi kuingilia kati ni lazima CDF atoe kibali na ithibitike kuna ulazima.
Kama uelewevyo kuomba Jeshi la Wananchi kuingilia kati ni lazima CDF atoe kibali na ithibitike kuna ulazima.
Hatimaye saa tisa za mchana kibali kilipatikana na Jeshi la Wananchi kwenda eneo la tukio.
Walipofika waliona kuna ulazima wa kutumia silaha nzito ili kulifumua pango hilo ili kujua kilichomo. Kuanzia hapo mizinga imekuwa ikisikika maeneo hayo ishara ya kwamba wanaume wapo kazini.
Walipofika waliona kuna ulazima wa kutumia silaha nzito ili kulifumua pango hilo ili kujua kilichomo. Kuanzia hapo mizinga imekuwa ikisikika maeneo hayo ishara ya kwamba wanaume wapo kazini.
Katika kuongeza nguvu kikosi maalumu kimeongezwa kutoka Dar ili kuhakikisha hali inakuwa salama.
Hadi jana asubuhi bado mizinga ilikuwa ikisikika licha ya kwamba kwa sasa haisikiki tena.
Hadi jana asubuhi bado mizinga ilikuwa ikisikika licha ya kwamba kwa sasa haisikiki tena.
Lengo la hao magaidi inasadikiwa ni kutoka kuwakomboa wenzao ambao wamefungwa au wapo magerezani.
Kwa mantiki hiyo, sakata kubwa lipo katika ulinzi wa Magereza ambapo wanasema ni wakati wa kulipa kisasi makubwa ambayo waliyataja ni Gereza Lilungu lililopo Mtwara, Gereza la Arusha na Gereza la Segerea lililopo Dar.
Pamoja na hayo bado ukweli unabaki wazi wanaweza kuvamia gereza lolote ili kutimiza malengo yao.
Pamoja na hayo bado ukweli unabaki wazi wanaweza kuvamia gereza lolote ili kutimiza malengo yao.
Ni jukumu sasa la vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha hali haiwi alijojo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni