Ni jambo la kawaida kwa mrembo au mtu yeyote anayeelewa masuala ya mitindo ya kunakshi vazi lake linapokuwa limekamilika.
Kwa kawaida vitu kama mikanda, mikoba, vibanio vya nywele hereni, hata cheni hutumika katika kupamba vazi la mtu husika.
Katika makala ya leo utaweza kufahamu jinsi hereni zinavyoweza kutumika kupamba vazi lako.
Wanawake wengi kwa sasa wamekuwa wakitumia hereni kupamba mavazi yao. Pamoja na ukweli huo ni wachache kati yao wanaoelewa namna sahihi ya kuvaa pambo hilo.
Mara kadhaa jambo hili limekuwa likisababisha kuharibika kwa mwonekano wa mhusika, wakati mwingine kushindwa kupata ujumbe kamili kutoka katika mavazi waliyovaa.
Kwa mfano; ukiacha uvaaji wa hereni za madini ya fedha na dhahabu, wanawake wengi wamekuwa wakitumia hereni za rangi kunakshi mavazi yao. Hili siyo wazo baya.
Lakini, tatizo hutokea pale mvaaji anaposhindwa kutambua ni mtindo upi wa hereni unaoendana na umbo lake, au vazi alilovaa na hapa ndipo mkanganyiko unapotokea.
Hiyo ndiyo sababu iliyowahamasisha wadau wa mambo ya mitindo kubuni dondoo muhimu za uvaaji wa hereni ikiwa ni moja ya mapambo muhimu kwa mwanamke.
Kuzingatia maumbo ni moja ya mambo muhimu katika fani ya urembo, kwani kwa kulijua vyema umbo lako, utaweza kujua au kujifunza; ni aina gani ya vitu vinavyoendana na mwili wako.
Katika uvaaji wa hereni, warembo wengi wamekuwa wakifanya makosa makubwa bila ya wao kujitambua na kuharibu mwonekano wao, ingawa wanaweza kuwa katika mavazi ya kuvutia na ya gharama.
Ukiwa mrembo, fuata ushauri ufuatao ili kwenda sawa ukitaka kujiweka katika hali ya kuvutia:
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni