Unyama wa kutisha! Mama mzazi aliyetajwa kwa jina la Feromena, mkazi wa
Meko-Mtongani, Kunduchi jijini Dar, anatuhumiwa kumcharanga viwembe
mwanaye wa kumzaa aliyetajwa kwa jina moja la Zena mwenye umri wa miaka
kumi.
Tukio hilo la kulaaniwa
lilijiri Jumanne wiki hii nyumbani kwa mwanamke huyo maeneo hayo ambapo
mama huyo inadaiwa alimsulubu mwanaye huyo anayesoma darasa la nne
katika Shule ya Msingi Mtakuja.
Kwa mujibu wa mashuhuda
wa tukio hilo, mama huyo alidaiwa kumfungia ndani mwanaye huyo na kuanza
kumpa kipigo cha mbwa mwizi.Walidai kwamba ukiachana na siku hiyo, mama
huyo amekuwa akimsulubu mwanaye huyo mara kwa mara kwa kumcharanga
viwembe na vitu vyenye ncha kali hivyo kumwachia majeraha sehemu
mbalimbali za mwili.
Sehemu ya majeraha yaliyo mgongoni mwa zena.
Mjumbe wa mtaa huo
aliyejitambulisha kwa jina la Elizabeth Mziga alikiri kupokea malalamiko
kutoka kwa majirani juu ya unyanyasaji na uteswaji wa mtoto Zena.Mjumbe
huyo alisema kuwa tuhuma hizo alishazifikisha polisi ambapo mama huyo
alikamatwa lakini baada ya muda alionekana akidunda mtaani kama kawa.
Mama mzazi wa mtoto Zena,Bi.Feromena akibanwa kwa maswali.
Baada kujazwa habari na
majirani na mjumbe huyo, kile kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu
cha Global Publishers kiliingia mzigoni ambapo kilianza kwa kumsaka
mtoto huyo na kuzungumza naye.
Alipopatikana, mtoto Zena
alieleza namna mama yake alivyokuwa akimfanyia matendo ya kinyama huku
akimnyima haki ya msingi ya kwenda shule.
Mama Zena, Bi. Feromena akiwa chini ya ulinzi.
Alisema mama yake amekuwa
akimtuhumu kumwibia fedha zake na kwenda kutumia shuleni hivyo
hakupaswa kurudi tena shuleni na kuongeza kuwa siku ambazo alikuwa
akilala kwa amani ni zile ambazo alikuwa ametoroka nyumbani na kwenda
kulala kwa majirani.
OFM ilishuhudia mwili wa Zena ukiwa na makovu na kuvimba huku akidai
kuwa aliunguzwa na ‘frampeni’ (kikaangio) hasa sehemu za kiunoni na
mgongoni.Alisema mama yake alimtishia kuwa endapo atamwambia baba yake
atakiona cha mtema kuni.
“Jamani mama amekuwa
akinipiga na kunikata viwembe bila kuniambia kosa langu. Naombeni msaada
nateseka,” alisema Zena kwa masikitiko makubwa.OFM, kwa kwa
kushirikiana na mjumbe wa eneo hilo walikwenda kuripoti tukio hilo
kwenye Kituo Kidogo cha Polisi cha Mtongani lakini hakukuwa na dawati la
jinsia hivyo polisi walikwenda kumkamata mama huyo kwa ajili ya
kumpeleka kituo kikubwa.
Moja ya wazee akionesha jalada la kesi aliyofunguliwa mama zena.
Kwa upande wake mama huyo
alipoulizwa sababu hasa ya kumsulubu mwanaye alisema si kweli bali
anachojua ni siku moja aliyompiga baada ya kuchukua fedha zake na kwenda
kununulia maandazi.
“Sijui aliyemkatakata viwembe,” alisema mama Zena kwa kifupi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni