promotion

Ijumaa, 16 Januari 2015

KIJANA ALIYEVUNJIKA MGUU KATIKA VURUGU ZA UDOM APATIWA MSAADA

mcharoman blogy
Kijana Iddy (mwanafunzi wa UDOM), aliyevunjika mguu katika vurugu za mgomo uliyofanywa na wanafunzi wa UDOM juzi.


Mguu wa kulia wa kijana Iddy ukiwa umevunjika.


KIJANA Iddy ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) aliyevunjika mguu katika vurugu za mgomo uliofanywa na wanafunzi wa UDOM Kitivo cha Sayansi ya Jamii juzi amepatiwa msaada wa matibabu na baskeli ya kutembelea walemavu 'wheel chair'.
Iddy ambaye amelazwa katika Hospitali ya General Dodoma, jana alipatiwa msaada wa fedha za matibabu pamoja na 'wheer chair' kutoka kwa Mhe. Shabiby baada ya kuzuiliwa kutoka hospitalini hapo kutokana na deni kubwa la matibabu aliyokuwa anadaiwa.
Mzazi wa kijana huyo ameeleza kuwa aliambiwa atapata msaada kutoka chuoni lakini cha kushangaza mpaka jana jioni alikuwa hajapata msaada wowote kutoka chuo cha UDOM zaidi ya kupigwa chenga na huku baadhi ya viongozi wakitupiana mpira.
Baba mzazi wa kijana huyo ametoa shukrani za pekee kwa Mhe. Shabiby aliyeguswa na kumsaidia kijana wake ambaye kwa sasa anaendelea vizuri.

Hakuna maoni: