promotion

Alhamisi, 25 Desemba 2014

Sikukuu ya Krismasi inachosha, inafundisha au ni ratiba?


Desemba 25 kila mwaka, Wakristo ulimwenguni kote huwa na sherehe za maadhimisho ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2,000 iliyopita.
Najua huu ni ujumbe wa kila mwaka, swali linalonisumbua daima ni, ujumbe huu wa Krismasi, unachosha, unafundisha au ni ratiba?
Kuna kitu kinachojengwa juu ya tukio hili la kila mwaka? Kuna hatua ya lazima katika maisha yetu inayosukumwa na tukio hili?
Twaweza kuishi na maisha yakaendelea kama kawaida bila tukio hili? Ni lazima kama ilivyo lazima kuishi? Ni lazima kama ilivyo lazima kuzaliwa, kukua, kula, kunywa, kusoma, kufanya kazi, kufurahi, kusikitika na hatimaye kufa?
Baba Mtakatifu Benedict wa 16 alihimiza imani pamoja na kufikiri. Lengo lake ni kwamba tunapoamini, tusitupilie mbali akili zetu.
Mungu katuumba na akili na kutupatia uwezo wa kutumia akili zetu kutafakari na kuvumbua vingine.
Jinsi tunavyovumbua vitu, ndivyo tunavyopaswa kutumia akili zetu kuvumbua mambo mengi yaliyojificha kwenye imani yetu kufuatana na nyakati tunazokuwamo.
Ndiyo maana, tumemsikia Baba Mtakatifu akitamka wazi kwamba si kila wakati kondomu inapotumika ni dhambi. Hata kama hakutamka na kusema.
“Kanisa linaunga mkono matumizi ya Kondomu,” kwa msimamo wake huo ni kwamba imani haiondoi akili, iko wazi kwamba siyo kila wakati matumizi ya kondomu ni dhambi.
Hili linatosha! Hata hivyo hakuna anayetaka kuitumia kondomu kwa matumizi mabaya ya kusababisha dhambi. Inatumika kama kinga ya kulinda uhai.
La msingi ni kuzingatia imani na kufikiri, imani na kutafakari, imani na kukubali baraka na Neema za Mwenyezi Mungu za kutuwezesha kugundua vitu mbalimbali na kuitumia sayansi na teknolojia iliyo kwenye dunia yetu.
Imani inakuwa na matukio mbalimbali. Mfano imani ya Kikristu ina matukio makubwa mawili; ya kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo na ina kufa na kufufuka kwake.

Hakuna maoni: