Wajumbe wa chama tawala cha National
Resistance Movement nchini Uganda wamepitisha mapendekezo ya kubadili
katiba yao na hivyo kumfanya katibu mkuu Amama Mbabazi kuwa hana kazi.
Mbabazi anafikiriwa kuwa ana nia ya kuwania Urais mwaka wa 2016 nchini Uganda dhidi ya rais wa sasa Yoweri Museveni.Moja wa wajumbe walioshiriki ni mbunge wa Soroti mjini Mashariki mwa Uganda na pia Makamu Mwenyekiti wa wa NRM kanda ya mashariki Mike Mukula ambaye anasema katika marekebisho katika katiba ya chama hicho, sasa katibu mkuu wa chama atakuwa akiteuliwa na mwenyekiti.
Pia naibu katibu mkuu na vilevile mweka hazina nafasi inayoshikiliwa na waziri wa biashara na ulimbikizaji Amelia Kyambadde, sasa watakaoteuliwa watakuwa watumishi wa kudumu wa chama bila kuteuliwa katika nafasi zingine serikalini.
Kuna waliokuwa wakipinga mabadiliko hayo na walikwenda mahakamani lakini mahakama ikatupilia mbali hoja hizo. Mjumbe Omar Kassim yeye anaunga mkono mabadiliko hayo.
Htaa hivyo mbunge Mukula anasem mabadiliko haya yanafanana kama chama tawala katika nchi jirani yaTanzania.
Kwa upande mwingine wajumbe wote elf 10 kila moja alipata pesa ambazo ni sawa na dola 180. Hii ni kwa naibu msemaji wa NRM Ofono Opondo Malazi pamoja na chakula cha wajumbe hao vililipwa na chama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni