Mkali wao katika Bongo Fleva, 'Diamond Platinumz' akiwa na Bi. mkubwa wake. |
WIKI iliyopita tuliishia pale Diamond alipokuwa hana kazi ya kufanya nyumbani hivyo alianza kutafuta vibarua mbalimbali vya kumuwezesha kupata riziki ya siku.Miongoni mwa kazi hizo ni kuuza mitumba, kuweka mafuta kwenye magari (vituo vya mafuta), kupiga picha, kupigisha simu na kazi za kwenye viwanda.Endelea sasa…
ACHEZA KAMARI
Wakati mwingine nyota huyo alijikuta akiingia kwenye makundi ya kucheza kamari za mitaani ili aweze kupata pesa ya kuingia studio kurekodi nyimbo zake. Hapo ni baada ya kujikubali kwamba anaweza.
Hata hivyo, michezo ya kamari haikumsaidia kwani alishindwa kufikia malengo yake.Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa Diamond. Alipenda kutoka lakini alishindwa atoke vipi!
AUZA PETE YA MAMA YAKE
“Hali ikazidi kuwa ngumu, ngumu, ngumu sana. Ilifika mahali nikaamua kuuza pete ya dhahabu ambayo mama yangu alinipa niivae. Nilimwongopea kwamba pete imedondoka. Aliniamini lakini kwa mbali sana.
“Kwa mauzo ya pete nilifanikiwa kupata fedha, nikaenda studio kwa mara ya kwanza kurekodi wimbo wangu wa kwanza kabisa uitwao Mawazo.
“Naamini kwa sababu ya uchanga kwenye fani sikuurekodi wimbo huu
katika viwango lakini ulianza kunikutanisha na watu mbalimbali ambao
walishangazwa jinsi nilivyoingia kwa mara ya kwanza studio na kukamua,
wao waliona kama mzoefu.”“Hali ikazidi kuwa ngumu, ngumu, ngumu sana. Ilifika mahali nikaamua kuuza pete ya dhahabu ambayo mama yangu alinipa niivae. Nilimwongopea kwamba pete imedondoka. Aliniamini lakini kwa mbali sana.
“Kwa mauzo ya pete nilifanikiwa kupata fedha, nikaenda studio kwa mara ya kwanza kurekodi wimbo wangu wa kwanza kabisa uitwao Mawazo.
AKUTANA NA MDHAMINI WA KWANZA
“Mdhamini wangu wa kwanza kabisa anaitwa Chizo, yeye alijitolea kunisimamia ili niweze kurekodi albamu nzima maana nilimwambia kwamba nina nyimbo nyingi,” alisema Diamond.
La kuvunda halina ubani, Diamond anasema kabla hajaweka mambo sawa, mfadhili wake huyo alipata matatizo, akawa hawezi kutoa fedha, hivyo ilimbidi aanze kuzunguka kwenye studio mbalimbali kuomba msaada wa kurekodiwa bure kazi zake.
Anasema baadhi ya studio (anazitaja majina) walimkatalia wakimwambia hajui kuimba, wengine hawakumpa hata nafasi ya kumsikiliza.
APIGWA CHINI NA DEMU WAKE
Diamond alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, ilifika mahali demu aliyekuwa naye (hakumtaja jina) alimwacha kwa sababu alikuwa akimpa ahadi hewa.
Demu huyo alichoshwa na maneno ya Diamond ya kila kukicha kwamba awe mvumilivu iko siku atatoka kisanii na watakuwa na maisha mazuri.“Kiukweli kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwangu maana hata yule mpenzi wangu alichoshwa na ahadi zangu hewa. Nilichanganyikiwa,” alisema Diamond.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni