Hali niliyonayo kiafya kwa sasa ni ya kutia mashaka, sina muda mrefu
kuendelea kuishi hapa duniani, nikifikiria ninavyoteseka ndani ya
familia yangu nikichanganya na maumivu ya ugonjwa usiopata matibabu,
naamini bila msaada wenu nitafariki dunia.”
Hajira Twalib Mdoka akiwa mwenye maumivu makali baada ya kuugua ugonjwa wa kansa.
NINACHOUGUA
Amesema ugonjwa unaomsumbua ni kansa, anajisaidia katika ndoo na kubebwa na baba yake baada ya kile alichodai mama yake kumkimbia.Alisimua jinsi anavyotaabika kama ifuatavyo:
“Mimi ni mtoto wa pili kuzaliwa kati ya watoto watatu, nilizaliwa bila tatizo lolote, nilipendwa na wazazi wangu hasa mama alikua kipenzi changu kuliko baba, leo hii mama kanikimbia ninatunzwa na baba ambaye anateseka kwa ajili yangu, najisikia vibaya anavyohangaika nami wakati hana kazi.
“Wakati nazaliwa wazazi wangu walikuwa wakiishi Mabibo CCM, Dar, baada ya kutimiza mwaka mmoja nilianza kutokwa na mabakamabaka miguuni kisha mwili mzima, utosini kukatokea kidonda baadaye vikaanza kuenea kichwani,vilianza kutoa funza, baba alinichukua hadi Hospitali ya Muhimbili, hapo sasa nikiwa na akili na kujijua.
Hajira Twalib akiwa amelala kitandani.
MSAADA WA JIRANI
“Tulirudi nyumbani, kwa bahati nzuri kuna jirani yetu mmoja alinionea huruma baada ya kusikia kuwa Muhimbili hawakunipa tiba yoyote wala vipimo, alimpatia baba shilingi laki moja na nusu ili nipelekwe Hospitali ya Ocean Road. Tulienda na iliwachukua muda mrefu bila kujua kinachonisumbua, baadaye waligundua kuwa ni kansa.
“Kulitokea uvimbe kwenye jicho la kulia, nilipigwa x-ray ambayo ilisababisha jicho kufa kabisa na kwa sasa halifanyi kazi na hili la kushoto nalo likawa halioni vizuri hadi sasa naona kwa shida tena kwa vitu vya karibu tu.
..Akinyweshwa soda na babu yake.
“Katika mkono wangu huu wa kushoto kuna kidonda kimetokea, baba aliambiwa atoe shilingi laki saba na nusu ili nifanyiwe upasuaji lakini hadi leo hii bado hajapata, hana uwezo kwani hata fedha ya kula inabidi baba akazunguke akiomba ndipo tupate kula.
SIPEWI DAWA ZOZOTE
“Ikawa tukienda Ocean Road tunapewa vidonge vya panadol tu, wakati fulani tunakosa fedha kwa ajili ya nauli, ilifikia hatua madaktari wakatueleza kwamba tukae nyumbani watakuwa wanakuja kunipa huduma lakini walikuja mara moja hawajarudi tena.
“Baba ananihangaikia kwa kila kitu, inapofika wakati wa kuniogesha hunimwagia maji bila kunisugua kwani akifanya hivyo mwili wangu humomonyoka, najisaidia kwenye ndoo, nakunywa uji kwa kutumia mpira, mdomo wangu unazidi kumomonyoka na kuna uvimbe umetoka katika sikio la kushoto, kichwa chote kimeoza, naumia sana (analia).
SIKU MAMA ALIPONIACHA
“Nakumbuka siku mama yangu anaondoka na kuchukua vitu vyote vya ndani na kuniacha bila maji wala chakula, baba alihangaika sana akawa anasaidiwa vitu kwa kupewa na majirani, kwa hali hii ya mateso makali sambamba na ugonjwa sitachukua muda mrefu, nitakufa kwa mateso bila kumuona mama.
Hajiraakiwa mtoto.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni