Wananchi
mkoani Njombe wameaswa kutoliingiza suala la tohara ya wanaume na imani
za dini kwa kuwa suala hilo ni kwa ajili ya kupunguza kasi ya
maambukizi ya virusi vya UKIMWI na manufaa mengine ya kiafya na si
vinginevyo
Hayo
yamebainika wakati wa uchangiaji mada iliyowasilishwa katika kikao cha
wadau wa mapambano dhidi ya vvu kilichoandaliwa na tume ya taifa ya
kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) ambapo imeonekana miongoni mwa changamoto
ambayo shirika la JHPIEGO lilikutana nayo wakati wa utekelezaji wa
huduma ya tohara ya wanaume ni imani ya dini
Mmoja
wa wachangiaji hao askofu mstaafu Dkt Peter Lukumbusho Mwamasika
ameeleza kuwa wapo baadhi ya watu wanadai wanaume wakifanyiwa tohara
wanakuwa wamehamishwa katika imani yao ya kikristo na kupelekwa katika
imani ya kiislamu jambo ambalo limepingwa vikali kuwa halina ukweli
wowote
Askofu
huyo amesema katika kipindi hiki ambacho kila mmoja anapambana na
maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi, tohara imegundulika kuwa ni moja
ya njia inayopunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa
waliofanyiwa tohara hivyo mwanaume aliyefanyiwa tohara imani yake ya
dini inabakia pale pale
Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayoshughulikia Ukimwi Mh. Lediana Mng'ong'o amewataka viongozi wa siasa kushirikishwa katika jitihada za kupambana na maambukizi ya VVU
"Humu ndani siwaoni madiwani,
siwaoni wenyeviti wa halmashauri, angalau nawaona wakuu wa wilaya,
wenyeviti wa halmashauri ndio wasimamizi wa sheria ndogondogo ninaomba
tuwashirikishe sana maana wanaushawishi mkubwa katika hili" amesema
Mng'ong'o
Amesema kwa nafasi hii wakishirikishwa viongozi wa siasa watakuwa wanapeleka taarifa hizo kwa wapiga kura wao suala hilo litasaidia kuwa na mabadiliko makubwa katika jamii
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni