Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akifafanua jambo mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali, kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaa,Mh.Sadick Meck Sadick akizungumza mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali, kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne.
Baadhi ya Watu wakishuhudia mabaki ya helikopta hiyo iliyopata ajali maeneo ya Kipunguni B Moshi Bar, Ilala jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya mabaki ya Helikopta baada ya kuanguka.
Baadhi ya Wataalamu wakifanya uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo ya Helikopta.
Muonekano wa Helikopta eneo la Gonga la Mboto jijini Dar.
Ajali ya Helicopter ya Maliasili na Utalii imegharimu maisha ya marubani 3 wa Jeshi la Polisi Tanzania. Sp Kidai Kaluse, Insp.Simba Must Simba, Pc. Josso Selestine, Na rubani mmoja Capt. Khalfan,Ajali hiyo imetokea huko Kipunguni B Moshi Bar,Ukonga-Ilala jijini Dar es Salaam. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikaa mpaka sasa.
Akizungumza na kituo cha ITV Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kutoa taarifa kamili juu ya tukio hilo muda mfupi ujao.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu @LazaroNyalandu ameandika hivi; “Naelekea Dar kutokea Dodoma kwenda kwenye eneo la tukio la ajali ili kuwapa pole wafiwa. Nitazidi kuwafahamisha.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni