Rapa wa Marekani Shawn Corey Carter a.k.a Jay Z ameingia kwenye headlines za vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na mitandao duniani.
Taarifa ikufikie kwamba baba wa Blue Ivy Carter na mume wa Beyonce, Jigga amenunua kampuni inayotengeneza Shampeni ya Armand de Brignac “Ace of Spades”.
Mapenzi ya Jay Z kwa Shampeni hiyo hayakuanza leo, katika ngoma yake ya “On to the Next” aliyoifanya na mkali Swizz Beatz aliwahi kuitaja Shampeni hiyo na katika kumpiga kampani Obama kwenye uchaguzi wa 2012 alizionyesha chupa 350.
Kampuni inayozalisha mvinyo huo ghali zaidi duniani haijasema kiasi cha fungu ambalo Jay kaweka kununua lebo ya Shampeni hiyo, ila mkwanja aliouweka unamhalalisha kuwa mmiliki wa Kampuni hiyo.
Jay ana utajiri wa dola mil. 520, mkwanja ambao anaukusanya unatokana na miradi yake ya nguo, migahawa na lebo ya muziki ya Roc Nation ambavyo vinamuweka kuwa tajiri wa tatu mwana Hip Hop duniani.
Alijibu hivi; “.. Ni kwa sababu ya bahati.. Mimi ni mtu mwenye bahati..”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni