Zaidi ya panya elfu nne wameuwawa ndani ya siku mbili katika hospitali maarufu ya serikali nchini India.
Mkurugenzi wa Hospitali hiyo amesema Kampuni ya kudhibiti wadudu imewaangamiza panya hao waliokuwa wakirandaranda katika majengo ya Hospitali hiyo ya Serikali.
Sanjay karmakar kiongozi wa kampuni ya Laxmi Fumigation and Pest Control Ltd amesema Hospitali ya Maharaja Yeshwantrao bado ina panya wengine elfu kumi katika maeneo ambayo operesheni hiyo haijafanyika.
Amesema Panya hao wamekuwa wakiwakamata kwa kuwatega na vitu mbalimbali kama Karanga, Viazi, Nyanya, Rosti ya Nyama na Njegere, Siagi, Keki vyakula ambavyo wanalazimika kubadili mara kwa mara kwani ikitokea panya wamekufa baada ya kula kitu kimojawapo siku hiyo, panya waliobaki huwa hawali wala kugusa.
Hospitali hiyo ni kati ya Hospitali kubwa za Serikali yenye uwezo wa kulaza wagonjwa miatisa na hamsini, ina Chuo cha mafunzo ya Udaktari ina wahudumia wagonjwa zaidi ya elfu moja na miamoja kwa siku.
Ubovu wa vifaa vya kuhifadhia taka umetajwa kuwa sababu ya kuwepo kwa panya hao kwa wingi katika hospitali hiyo na Operesheni hiyo imeanza Oktoba 28 na inategemea kumalizika Desemba4 ingawa wamekuwa hawafanyi zoezi hilo mara kwa mara jambo ambalo limekuwa likichangia panya hao wasiishe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni