Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM na mlezi wa mkoa wa Simiyu Jerry Silaa akiongea na wananchi wa kijiji cha Mwamhongo wilayani Meatu, mkoa wa Simiyu. Ndg. Jerry Silaa amechangia mabati 50 kusaidia ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Mwamhongo kata ya Mwasengela kilometa 94 toka makao makuu ya Wilaya ya Meatu. Ndg.Jerry amekuwa kiongozi wa kwanza wa Chama chochote wa ngazi ya Taifa kukanyaga ardhi ya Kijiji hiki.
Ujenzi wa barabara za lami kilometa 3 kwenye mji wa Mwanhuzi makao makuu ya Wilaya ya Meatu. Kazi imefanyika kwa asilimia 40 na itakamilika mwezi wa tatu mwakani.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni