INDIRA Priyadarshini Gandhi; alikuwa Rais wa India. Aliuawa mwaka1984 kwa kupigwa risasi na walinzi wake, Satwant Singh na Beant Singh jijini New Delh, India.
JOHN Francis Kennedy ‘JFK’; ni Rais wa 35 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1963 mjini Dallas kwa kupigwa risasi na Lee Harvey akiwa kwenye gari la wazi barabarani.
LAURENT Desire Kabila; alimng’oa madarakani Rais Mabotu Seseko wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, lakini mwaka 2001 akauawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa ni walinzi wake.
THOMAS Isdor Noel Sankara; alikuwa Rais wa Burkina Faso Alitawala nchi kwa miaka 4 hadi 1984 alipouawa kwa kupigwa risasi na Blaise Compaore ambaye hivi karibuni ameikimbia nchi hiyo.
WILLIAM Richard Tolbert Jr; alipigwa risasi mwaka 1980 katika mapinduzi ya kijeshi akiwa Rais wa Liberia. Samuel Doe akiwa na cheo cha sajenti ndiye aliyetajwa kumuua.
MUHAMMAR Muhamad Abu Migar al Ghaddaf; alikuwa Rais wa Libya kwa miaka 42. Aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa kwenye vurugu za kisiasa mjini Sirte, Libya, Oktoba 20, 2011.
ABEID Amani Karume; alikuwa Rais wa Zanzibar tangu mapinduzi ya mwaka 1964. Aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa anacheza bao mwaka 1972 na mtu ambaye hakuwahi kupatikana.
Jean baptist ouedraogo; aliitawala Burkina Faso kwa mwaka mmoja tu, 1982-83. Aliuawa kwa kupigwa risasi na Thomas Sankara ambaye alichukua madaraka ya kuiongoza nchi hiyo kabla na yeye kupinduliwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni