promotion

Ijumaa, 14 Novemba 2014

Mfumo wa Tancis wasaidia kuondoa urasimu, wizi bandarin



MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema mfumo mpya wa forodha wa kielektroniki (Tancis) umesaidia kuondoa urasimu na wizi wa makontena Bandarini.
Ofisa Mwandamizi wa TRA, Felix Tinkasimile, alisema hayo katika mkutano wa wadau wa usafirishaji sekta ya maji ulioandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri nchi kavu na Majini (SUMATRA) kujadili changamoto na faida za mfumo huo.
Tinkasimile alisema mbali na urasimu pia mfumo huo umeongeza ukusanyaji wa kodi Serikali kutokana na kutoruhusu udanganyifu na wizi katika utaratibu wa kusafirisha mizigo.
Alisema kabla ya kuanza kwa mfumo huo TRA na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ilikuwa ikikabiliwa na kesi nyingi za upotevu wa makontena bandarini jambo ambalo kwa sasa halipo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamunyange, alisema mfumo huo ni sehemu ya mikakati ya serikali katika kuhakikisha matokeo makubwa sasa (BRN) inafanikiwa katika sekta ya Meli.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Gilliard Ngewe, alisema nia ya kuandaa mkutano huo ni kutokana na malalamiko kadhaa waliyopata toka kwa wadau hao tangu kuundwa kwa mfumo huo hivyo kuwataka TRA kufika na kutoa ufafanuzi.

Hakuna maoni: