CHAMA Kikuu cha Ushirika Mkoa Kagera (KCU 1990) Ltd, kimewachagua viongozi wapya huku wa zamani wakitoshwa katika mkutano mkuu maalum uliofanyika mjini hapa, juzi.
Uchaguzi huo umefanyika chini ya usimamizi wa Mrajisi Msaidizi wa Mkoa Kagera, Rweikiko Shorosi, ambaye alisema serikali inapenda kuona vyama vya ushirika vikifanya vizuri.
Alibainisha migogoro inayovikumba vyama vya ushirika, inakwamisha harakati za wananchi kutafuta fursa za kujiwezesha kimaendeleo.
Alisema watu 22 waliojitokeza kuchukua fomu kuwania Ujumbe wa Bodi ya KCU 1990, na majina yaliyorudi baada ya kuchujwa ni 18, wote wakiwa sura mpya tofauti na walivyotarajia watu wengi.
Katika nafasi ya Mwenyekiti, Frank Muganyizi alishinda akipata kura 189 kati ya 246 zilizopigwa huku Sylvanus Muhyoza akipata kura 50.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Ingatus Batanuzi alishinda kwa kura 136 akiwabwaga Festo Paulo kura 31, Sandru Nyangasha kura 78.
Wajumbe wapya waliochaguliwa ni Winfrida Kyombo (102), Festo Paulo (56), kutoka Missenyi, Sylvanus Muyoza (227), Bukoba, Ignatus Batamuzi (133), na Projestus Balengela (44), Muleba.
Wilaya ya Bukoba waliochaguliwa ni Sandru Nyangasha (60), na Frank Muganyizi (90), pia wajumbe hao walimchagua Dominick Kasaju kutoka Chama cha Msingi Bukwali wilayani Missenyi kuwa mwakilishi kutoka nje ya bodi baada ya kupata kura 182.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Mrajisi Msaidizi, Moshi Chogero, alisema umefanyika kwa mujibu wa sheria namba sita ya mwaka 2013 na ni uhuru na haki.
Alisema kwa wajumbe ambao walichukua fomu na kujaza lakini majina yao hayakuweza kurudi, wanaweza kukata rufaa kwa mrajisi kwani ni haki yao ya kidemokrasia kufanya hivyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni