promotion

Jumanne, 25 Novemba 2014

Breaking News!! HIACE YA KAHAMA-SHINYANGA YAUA WATU HIVI PUNDE KONA YA BUHANGIJA MJINI SHINYANGA



Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio-
Gari ikiondolewa eneo la tukio
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Dkt Anselm Tarimo akiwa na maafisa wa polisi mkoa wa Shinyanga eneo la tukio-
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio-Pi

Watu watano wanadaiwa kupoteza maisha  leo majira ya saa tano asubuhi baada ya gari ndogo Hiace yenye namba za usajili T761 CKD ikitoka Kahama kwenda Shinyanga Mjini kupinduka katika eneo la Kona ya Buhangija mjini Shinyanga.

Walioshuhudia wanasema hiace hiyo ilikuwa katika mwendo kasi ikifukuzana na Hiace nyingine ndipo ikamshinda dereva wake baada ya kupiga Bamz ya Buhangija na kupinduka mara tatu.

Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema wameondoa miili mitano ya marehemu katika gari hiyo.
Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Tutakuletea taarifa kamili hivi punde kuhusu idadi kamiliya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo na idadi ya majeruhi.






picha na malunde blog

Hakuna maoni: