Bibi harusi Mariamu Mduwa aliyenusurika katika ajali ya mitumbwi katika kijiji cha kalalangabo akiwa anaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa wa Kigoma |
WATU sita wamekufa maji katika ziwa Tanganyika na wengine 11 kunusurika kifo akiwemo bwana harusi Shaaban Idd na bibi harusi
Mariamu Mduwa baada ya mitumbwi miwili waliyokuwa wakisafiria kutoka kigoma mjini kwenda katika kijiji cha Kigalye kilichopo mwambao mwa ziwa Tanganyika kuzama ziwani.
Tukio hilo limetokea jumamosi saa nane na nusu mchana baada ya mitumbwi hiyo kupigwa wimbi kali na kuzama katika kijiji cha Kalalangabo wakati bwana harusi huyo akitoka kuoa katika eneo la mwandiga na kurudi nyumbani akiwa na ndugu na jamaa pamoja na wapambe.
Akiongea na blog hii katika wodi namba 5 katika Hospital ya Mkoa wa Kigoma alipolazwa bibi harusi huyo alisema kuwa alishikwa na bumbuwazi sana baada ya tukio hilo kwani mpaka sasa bado hajielewi.
Ndugu, jamaa na wapambe wa bwana na bibi harusi walionusurika katika ajali ya mtumbwi katika kijiji cha Kalalangabo wakiwa wanaendelea na matibabu katika hospita ya Mkoa wa Kigoma
''Sikumbuki kitu kwani baada ya mtumbwi kuzama kila mtu alikuwa anahangaika kujiokoa na kifo.
"kwakweli mimi naona kama mkosi siku ya harusi yangu watu wanakufa ila namshukuru Mungu kwa kutunusuru na kifo na yote mimi nimemwachia Mungu''alisema bibi harusi huyo
Mwathirika mwingine aliyenusurika katika ajali hiyo Zabibu Issa alisema kuwa mitumbwi waliyokuwa wamepanda ilikuwa imejaza sana watu na mizigo ndiyo maana ilizidiwa uzito na kuzama baada ya kupigwa na wimbi.
''Safari ya kwenda kijijini kwetu lazima tupite njia za majini hakuna barabra kabisa sababu vijiji tunavyoishi vipo mwambao mwa ziwa Tanganyika kungekuwa na barabara tungepita barabrani''alisema Bi Zabibu Issa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni