Kisonono ni ugonjwa wa zinaa naoambukizwa, ugonjwa huu hutokana na wadudu aina ya Neisseria gonorrhoeae. Ugonjwa huu pia huambukizwa kwa tendo la ngono na hata kutoka kwa mama mjamzito anapojifungua huweza kumuambukiza pia mtoto endapo atakuwa alikuwa nao.
Ugonjwa wa kisonono kwa mara nyingi huwapata vijana na watu wazima. Waathirika wengi wa ugonjwa huu wa kisonono huambatana na magonjwa mengine ya zinaa, kwasababu kunabaadhi ya magonjwa mengine ya zinaa hujificha bila kuonyesha dalili, hivyo kukuta ukiugulia ndani kwa ndani.
Ugonjwa wa kisonono, unazuilika na kutibika pia, unaposikia dalili zozote za magonjwa ya zinaa, unashauriwa kumchukua mwenzi wakona kuwahi hospitali kuchukua vipimo kwaajili ya matibabu.
DALILI ZA UGONJWA WA KISONONO.
Mara nyingi ugonjwa wa kisosnono huwa hauonyeshi dalili yoyote mwanzoni. Lakini ukionyesha dalili basi kwa mwanaume utasikia maumivu makali wakati wa kukojoa na kuambatana na usaha kutoka uumeni, kwa mwanamke pia dalili ni hizo hizo - maumivu wakati wa haja ndogo na kutoa usaha ukeni.
Usaha huo unaotoka uumeni au ukeni, huwa mzito na rangi ya kijani-njano, ambapo kwa mwanaume anaweza kuhisi maumivu katika korodani zake. Kwa Wanawake maumivu yanaweza kuwachini ya tumbo, uchungu wakati wa ngono, na damuIsiyokuwa ya kawaida kutoka kwenye uke.
Kama
Katika wanawake, kisononokinaweza kusababisha zaidikutoka eneo la uke na kusababisha papo hapo ugonjwa mwingine wa "pelvicinflammatory" (PID) -maambukizi katika maeneo mbali mbali ya uzazi yanaweza kusababishautasa.
Katika wanaume na wanawake, kisonono kisichotibika kwa muda muafaka, huenda huweza kuenea kupitia damu katika sehemu za mwili ambazo ni mbali na viungo vya uzazi,na kusababisha uvimbe katika viungo, ngozi, mifupa, tendons, moyo, au hata eneo karibu na ini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni