mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Wanasiasa sita waandamizi wamefurushwa kutoka kwa serikali ya muungano katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo baada ya kumuandikia rais wakimtaka kutokwamilia madaraka, kulingana na maafisa.
Katika barua kwa Joseph Kabila,viongozi wa G7,kundi lenye vyama ndani ya muungano huo lilitaka hatua kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kufikia mwezi Novemba.
Mda wa kikatiba wa rais Kabila unakamilika mwaka ujao,lakini amekataa kuthibitisha kwamba hatowania muhula mwengine.
Upinzani pia unahofia kwamba uchaguzi huo utacheleweshwa.
Ulifanya mkutano wa kisiasa katika mji mkuu wa Kinshasa hapo siku ya jumanne ili kumtaka rais Kabila ajiuzulu mwaka ujao.
Msemaji wa serikali Lambert Mende alikana kwamba bwana Kabila alitaka kukiuka katiba kulingana na n chombo cha habari cha Reuters.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni