promotion

Jumatano, 30 Septemba 2015

Undani wa vifo vya familia ya watu watano iliyokatwakatwa mapanga wilayani maswa mkoani simiyu

mcharoman blog fahar yako mtanzania


Tukio la kinyama la watu 5 wa familia moja kukatwa katwa mapanga kisha kupoteza maisha papohapo lililotokea katika Kitongoji cha Kisesa kata ta Bugalama wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu limegubikwa na utata mkubwa juu ya wahusika na chanzo cha tukio hilo.

Makabuli ya watu watano waliouawa kwa kukatwa katwa mapanga  kama wanyama katika Kitongoji cha Kisesa kata ya Bugalama wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.



Tukio hilo lililotokea juzi majira ya saa 9:00 usiku na kuripotiwa katika vyombo vya habari, lilihusisha Baba, Mama pamoja na watoto 3 kutendewa unyama huo, huku chanzo kikielezwa na jeshi la polisi kuwa ni mgogoro wa ardhi.

Timu ya waandishi wa habari iliyofika katika Kitongoji hicho na kuongea na baadhi ya wananchi, majirani pamoja na ndugu na wazazi wa marehemu ilibainikuwa kuwa chanzo kilichotolewa na jeshi la polisi siyo sahihi.

Walieleza kuwa chanzo hicho cha tukio kinachoelezwa kuwa sababu ya familia hiyo kutendewa unyama huo, hakina ukweli wowote kutokana na familia hiyo kuifahamu fika undani wake pamoja na maisha waliyokuwa wakiishi kijijini hapo.

Katika chanzo hicho kilichotolewa na jeshi la pilisi kilieleza kuwa ni Mgogoro wa ardhi kati ya marehemu (George, Baba wa familia) pamoja na Baba yake wa kambo ambaye alinunua kipande cha ardhi alikokuwa akiishi marehemu.

Portini Shili ni Jirani wa familia iliyouawa ambapo anaeleza kuwa chanzo hicho siyo kweli kutokana na kufahamu ukweli wa upatikanaji wa eneo hilo ambalo lilielezwa kuwa sababu ya tukio hilo.

“ hilo eneo wanaloeleza polisi lilikuwa ni eneo la Mpwa wangu (mtoto wa dada yangu) wakati wanauziana eneo hilo mimi nilikuwepo…aliuziwa baba wa kambo wa marehemu (George)…lakini wakati ananunua eneo hilo tayari familia hii iliyouawa walikuwemo katika eneo hilo na wanaishi” Alisema

Aliongeza kuwa mpwa wake kabla ya kuuza eneo hilo alimkaribisha marehemu pamoja na familia yake ili kuishi ambapo, familia hiyo iliweza kujenga nyumba ikiwa pamoja na kuanzisha duka lililokuwa na bidhaa nyingi kuliko maduka mengine Kitongojini hapo.

Alisema wakati zoezi la kununua eneo hilo familia hiyo tayari ilikuwa inaishi na hapakuwepo mgogoro juu ya kuwemo ndani ya eneo wakati likiuzwa, huku akieleza kuwa baba wa kambo Migata Lusalago alimruhusu kuendelea kukaa eneo hilo mtoto wake pamoja na familia yake.

“ hakuna ukweli juu ya chanzo hiki…lakini Baba wa kambo ambaye anatuhumiwa na amekamatwa alikuwa mzee mwenye heshima hapa kijijini…mimi nilikuwa ndani ya familia hiyo mapenzi kwa mtoto wake yalikuwa makubwa sana kutokana na kuwasadia” Alisema Shili

Mbali na jirani huyo mzazi wa mama wa familia John Lutamba, ndugu wa marehemu (Zengwe Sendama, mjomba (Renatus Dutu) walieleza kuwa chanzo hicho siyo kweli kutona na kuishi vizuri na familia hiyo huku wakikana kutokuwepo kwa mgogoro wa ardhi katika familia yao.

“ Hakuna ukweli wa juu ya chanzo hicho…mpaka sasa tupo tunajiuliza nini chanzo…na wahusika ni akina nani?...na hakuna mwenye jibu…katika familia yetu hakuna mgogoro wowote wa ardhi na tulikuwa tunaishi vizuri” Walisema
Akiongelea tukio hilo Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Bugalama Christopher Kulwa alisema kuwa tangu amekuwa kiongozi katika kijiji hicho hajawahi kusikia au kuletewa ugonvi au mgogoro juu ya familia hiyo.

Alisema kama uongonzi wa serikali ya kijiji bado unafuatilia chanzo pamoja na wahusika katika tukio hilo, ambapo alieleza katika hatua za awali za uchungunzi waliamu kila kila mwananchi katika kitongoji hicho kupiga kura za siri.

“ tumeendesha kura ya siri kwa kila mtu kwa ambaye anaweza kufahamu wahusika na chanzo…kura hiyo tayari tumepatiwa baadhi ya majina ya watu ambao walikisiwa kuhusika…na tunayafanyia kazi kwa kushirikiana na jeshi la polisi” Alisema Mwenyekiti

Baadhi ya wananchi ambao hawakutaka kutajwa majina yao wakiwemo watu wa karibu walisema kuwa chanzo ambacho kinaweza kusababisha tukio hilo ni kujituma na kujishughulisha kwa Marehemu baba wa familia kutokana na kuoneka kuwazidi wananchi wengine kifedha kijijini hapo.

“ Marehemu alikuwa na duka kubwa hapa kijijini…alikuwa na roho nzuri…anakopesha kila mtu…lakini kila bidhaa ilikuwa ikipatikana kwake…alikuwa amefunga umeme wa sola nyumbani kwake…mbali na hayo alikuwa akiwazidi wenzake katika mahuzo hapa kijijini” Alisema mmoja wa wanakijiji.

Kauli hiyo ilionekana kuungwa mkono na Mjomba wa Marehemu baba wa familia Renatus Dutu kwa maelezo kuwa kutokana na juhudi zake inawezekana baadhi ya wanakijiji walikuwa hawataki.

“ nyumba yake ndiyo ilikuwa na umeme tu hapa kijijini…alikuwa akichaji simu nyingi za wananchi…duka lake lilikuwa kubwa…tuna hofu juu uwezo wake huo unaweza kuwa chanzo…lakini natambua kuna baadhi ya watu wametajwa tena baadhi yao ni vijana tunalitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo vizuri” Alisema Dutu

Hata hivyo katika uchunguzi huo ilibainika kuwa chanzo kinaweza kuwa wivu kutoka kwa wanafamilia na wanakijiji hasa vijana kutokana na Marehemu baba wa familia kuwa na duka kubwa katika kitongoji hicho, huku akiwazidi uwezo wa kifedha na kimaendeleo ndugu zake.

Waliouawa kwa kukatwa katwa mapanga katika tukio hilo ni George Charles (30) ambaye ni Baba wa familia, Siku John (23) Mama wa Familia na watoto wao ambao ni Mchambi George (7) Tuma George (5) pamoja na Amos George (Miezi 9) wote wasukuma wa kitongoji hicho.

 SOURCE SIMIYU NEWS



Hakuna maoni: