mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Baadhi ya wanawake waliojitokeza katika hafla hiyo wakiwa katika viwanja vya Karimjee, Dar.
Sehemu waliyokuwa wamekaa baadhi ya wanawake kutoka vyama mabalimbali vya siasa waliojitokeza katika kinyanganyiro cha uchaguzi.
...
mkutano ukiendelea.
B
aadhi ya akina mama waliojitokeza kwenye mkutano huo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Samiah.
Kutoka kulia ni mgombea mwenza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samiah Hassan Suluhu, Mama Anna Abdallah na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi.
Samiah Suluhu akizungumza jambo katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake, Katiba na Uchaguzi, Prof. Ruth Meena (kushoto) akizungumza jambo.
Prof.Ruth Meena (kushoto) akimkabidhi Samiah Suluhu ilani ya uchaguzi, anayeshudia katikati ni Mama Anna Abdallah.
Mwenyekiti wa ulingo wa mtandao wa wanawake mama, Anna Abdallah akizungumza jambo katika mkutano huo.
MTANDAO wa Wanawake na Katiba, leo Jumatatu umemkabidhi mgombea mwenza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samiah Hassan Suluhu, ilani ya uchaguzi itakayomuongoza katika utekelezaji wake wa shughuli za kuleta maendeleo baada ya uchaguzi mkuu mwaka huu kumalizika.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Samiah Suluhu ambaye pia ndiye alikuwa mgeni rasmi, amesema kuwa mtandao wa wanawake na katiba ni mtandao ambao unatoa fursa kwa wanawake kutoka vyama vyote vya siasa bila kujali itikadi zao huku lengo likiwa ni kuhakikisha wagombea wote wanaheshimu na kupigania nafasi ya mwanamke katika kuleta maendeleo hapa nchini.
Aidha alisema kuwa amefurahishwa na namna mtandao huo unavyowajali wanawake. Akaongeza kwa kusema amefurahishwa namna wanawake wengi walivyojitokeza katika kuwania nafasi mbalimbali za kugombea uongozi hivyo sasa ni wajibu wao kuhakikisha wanadumisha umoja na mshikamano katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Amesema kuwa wanawake wakiamua kufanya jambo wanaweza, hivyo sasa ni wajibu wao kuhakikisha wanajikwamua kwa kufanya biashara japo ndogondogo ambazo zinaweza kuwasaidia kujikwamua kimaisha.
Samiah amewataka wanawake kuwa waaminifu wanapokuwa katika ajira za taasisi binafsi na serikalini, kufanya shughuli zao za kila siku kwa kuzingatia sheria stahiki
(PICHA / HABARI: DENIS MTIMA/GPL)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni