mcharoman blogy fahar yako mtanzania
JESHI LA POLISI WILAYANI BARIADI MKOANI SIMIYU LIMEMFIKISHA MAHAKAMANI MKAZI MMOJA WA KIJIJI CHA NKOLOLO WILAYANI BARIDI KWA TUHUMA YA KUMBAKA MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA NA KUMSABABISHIA UJAUZITO.
MSHITAKIWA ALIYEFIKISHWA MAHAKAMA YA WILAYA YA BARIADI MBELE YA HAKIMU WA MAHAKAMA YA MKOA WA SIMIYU JOHN NKWANI NI YOHANA SAGUDA (19) MKAZI WA KIJIJI CHA NKOLOLO KATA YA NKOLOLO WILAYANI BARIADI.
IMEDAIWA NA MWENDESHA MASHTAKA WAKILI WA SERIKALI MAFURU MOSES KUWA MSHITAKIWA ALITENDA KOSA HILO NOVEMBA 16 MWAKA JANA MNAMO MAJIRA YA SAA 11 JIONI AKIWA NYUMBANI KWAKE HUKO KATIKA KIJIJI CHA NKOLOLO.
AMBAPO ALIENDELEA KUFANYA UBAKAJI HUO HADI MWANAFUNZI HUYO ALIPOGUNDULIKA NA UJAUZITO MARCH MWAKA HUU.
AMESEMA MTUHUMIWA ALIMBAKA MSICHANA ALIYEKUWA AKISOMA DARASA LA SABA JINA (LINAHIFADHIWA) KATIKA SHULE YA MSINGI NKOLOLO ‘A’ AKIMWAHIDI KUMSAIDIA KIMASOMO KWA KUWA YEYE AMEHITIMU KIDATO CHA NNE.
HUKU AKIMTAKA MWANAFUNZI HUYO KUWA ANAKWENDA NYUMBANI KWAKE KWA LENGO LA KUMFUNDISHA MASOMO YA ZIADA KILA JIONI ANAPOTOKA SHULE.
WAKATI MWANAFUNZI HUYO AKIENDA NYUMBANI KWA KIJANA HUYO ALIKUWA AKILAZIMISHWA KUFANYA TENDO LA NGONO HALI ILIYOPELEKEA KUMSABABISHIA UJAUZITO NA KUSHINDWA KUENDELEA NA MASOMO.
HAKIMU MKAZI MWANDAMIZI MFAWIDHI WAMAHAKAMA YA MKOA WASIMIYU JOHN NKWABI AMEIHARISHA KESI HIYO HADI SEPTEMBA 17 MWAKA HUU KWA AJILI YAKUENDELEA NA UTETEZI UPANDE WA MSHITAKIWA.
MTUHUMIWA YUKO NJE KWA DHAMANA BAADA YA KUKIDHI MASHARTI YA DHAMANA.
STOR NA
ABDALLAH- NSABI-SIMIYU
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni