mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Walimu hao wapatao 30, wamemlalamikia mkuu huyo na kudai kuwa hatua yake yenye madai ya kuwatishia kuwatimua kazi ni kinyume cha haki yao ya kikatiba na sheria.
Wakiongea na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mara baada ya kumalizika kwa kikao chao na viongozi wa Chama Cha Walimu
Tanzania (CWT), wilayani humo, walisema kuwa kitendo cha Kirigini kuwaita baadhi ya walimu na kuwatishia kuwafukuza kazi kwa madai ya kushabikia vyama vya upinzani ni uongozi wa kidkiteta na umepitwa na wakati.
Walidai kuwa kitendo hicho cha kiongozi wa serikali ni matumizi mabaya ya madaraka huku wakisisitiza kuwa ni haki yao kuwa na itikadi ya kisiasa bila kuchaguliwa na mtu huku wakisisitiza kuwa hawaruhusiwi kufanya siasa wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi.
Hata hivyo, walisema wameshangazwa na kitendo cha kutuhumiwa bila kupewa nafasi ya kujieleza, licha ya kuwapo kundi kubwa la baadhi ya walimu wilayani humo ambao ni viongozi ndani ya chama tawala cha CCM ambao ameshindwa kuwaonya.
Aidha walimu wametaka wasiingiliwe kwenye uhuru wao binafsi kwani hakuna mwenye hati miliki na nchi.
Kwa upande Kirigini alikiri kuwaonya walimu 30 baada ya kupata taarifa kuwa wanajihusisha na siasa jambo ambalo halitakiwi kwa mtumishi wa serikali.
“Ni kweli niliwaita walimu hao na kuwaonya kuacha kujihusisha na masuala ya siasa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na wapo wengine walijitokeza katika kura za maoni katika vyama vya upinzani nami nilifanya hivyo baada ya kupata taarifa za mienendo yao, alisema.
STORY NA ANCETH NYAHORE
Baadhi ya walimu katika Wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu, wamemtaka Mkuu wa wilaya hiyo, Rosemary Kirigini, kuacha tabia ya kuwatisha kwa madai kuwa wanashabikia vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).Walimu hao wapatao 30, wamemlalamikia mkuu huyo na kudai kuwa hatua yake yenye madai ya kuwatishia kuwatimua kazi ni kinyume cha haki yao ya kikatiba na sheria.
Wakiongea na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mara baada ya kumalizika kwa kikao chao na viongozi wa Chama Cha Walimu
Tanzania (CWT), wilayani humo, walisema kuwa kitendo cha Kirigini kuwaita baadhi ya walimu na kuwatishia kuwafukuza kazi kwa madai ya kushabikia vyama vya upinzani ni uongozi wa kidkiteta na umepitwa na wakati.
Walidai kuwa kitendo hicho cha kiongozi wa serikali ni matumizi mabaya ya madaraka huku wakisisitiza kuwa ni haki yao kuwa na itikadi ya kisiasa bila kuchaguliwa na mtu huku wakisisitiza kuwa hawaruhusiwi kufanya siasa wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi.
Hata hivyo, walisema wameshangazwa na kitendo cha kutuhumiwa bila kupewa nafasi ya kujieleza, licha ya kuwapo kundi kubwa la baadhi ya walimu wilayani humo ambao ni viongozi ndani ya chama tawala cha CCM ambao ameshindwa kuwaonya.
Aidha walimu wametaka wasiingiliwe kwenye uhuru wao binafsi kwani hakuna mwenye hati miliki na nchi.
Kwa upande Kirigini alikiri kuwaonya walimu 30 baada ya kupata taarifa kuwa wanajihusisha na siasa jambo ambalo halitakiwi kwa mtumishi wa serikali.
“Ni kweli niliwaita walimu hao na kuwaonya kuacha kujihusisha na masuala ya siasa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na wapo wengine walijitokeza katika kura za maoni katika vyama vya upinzani nami nilifanya hivyo baada ya kupata taarifa za mienendo yao, alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni