mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Taarifa za awali ambazo zimetoka kwa wananchi waliokuwa wakishuhudia tukio hilo wanasema kuwa mwanamke huyo alikuwa akivuka mto katika mtaa huyo, ambapo walieleza kuwa yawezekana wakati akivuka gfla fisi huyo alimkaba kisha kumuua.
Mkuu wa wilaya ya Bariadi Mkoani hapa Ponsian Nyami akiongea na waandishi wa habari kudhibitisha kutokea kwa tukio hilo, alisema kuwa bado hajapata taarifa rasmi lakini alisikia kutoka kwa watu.
SOURCE SIMIYU YETU
Ni tukio ambalo linasadikika kutokea jana majira ya jioni, mwanamke mmoja mkazi wa Bariadi jana amefariki dunia baada ya kuliwa na fisi katika Mtaa wa kidinda uliko Mjini Bariadi.
Taarifa za awali ambazo zimetoka kwa wananchi waliokuwa wakishuhudia tukio hilo wanasema kuwa mwanamke huyo alikuwa akivuka mto katika mtaa huyo, ambapo walieleza kuwa yawezekana wakati akivuka gfla fisi huyo alimkaba kisha kumuua.
Hata hivyo uchunguzi wa kifo cha mwanamke huyo umeleta utata, baada ya baadhi ya watu kudai kuwa siyo kawaida fisi kuweza kumsabaishia kifo mtu mzima, na badala yake fisi wamekuwa wakiwakamata watoto wadogo.
" kwa kawaida na hili litakuwa tukio la kwanza hakuna fisi ambae anaweza kumkamata mtu mzima...tunavyofahamu walio wengi fisi uwakamata watoto wadogo watu wazima huwa anawaogopa...inakuwa je kwa huyu mama tena mtu mzima? ninavyofikiri mwanamke huyu aliuawa na mtu kisha akatupwa maeneo haya na fisi wakati wa pita pita zao wakamkamata" Alisema mmoja wa waananchi.
Ikiwa itadhibitika kuwa mama huyo aliuawa na fisi, basi matukio ya wanayama hao kuwasababishia watu vifo yatakuwa yamekidhiri, kutokana ndani ya mwezi mmoja (Agost) jumla ya matuki 3 yametokea mjini Bariadi huku mawili kati hayo ni watoto kuuawa na fisi na moja la mwanamke huyo.
Mkuu wa wilaya ya Bariadi Mkoani hapa Ponsian Nyami akiongea na waandishi wa habari kudhibitisha kutokea kwa tukio hilo, alisema kuwa bado hajapata taarifa rasmi lakini alisikia kutoka kwa watu.
Alisema kuwa taarifa tayari zimepelekwa polisi na bado katika ofisi yake hazijafika ambapo alibainisha kuwa ataitisha kikao baina yake na maafisa maliasili kuona jinsi gani ya kaunza msako wa kuwakamata fisi.
Kwa upande wa jeshi la polisi viongonzi wote wa ngazi za juu hawakuwepo ofisini kutokana na kuwa na kazi maalumu ya ukaguzi.
Endelea kutembelea mtanado huu, ili kuweza kupata habari zaidi juu ya tukio hili hapo kesho, mabapo jeshi la polisi litatoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari.
Imeshindikana kuwaletea picha za mama huyo ambaye mpaka sasa hajaweza kutambulika jina wala makazi yake, kutokana na kutokuruhusu kimaadili.
SOURCE SIMIYU YETU
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni