mcharoman blogy fahar yako mtanzania
via ikulu mawasiliano
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Said
Meck Sadik kufuatia vifo vya watu tisa wa familia moja ya Bwana Masoud Matal
vilivyotokea alfajiri ya tarehe 27 Agosti, 2015 kwa ajali ya moto.
Wanafamilia
hao wakiwemo watoto watano walipoteza maisha baada ya nyumba yao iliyoko katika
Mtaa wa Gulam, eneo la Buguruni Malapa katika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es
Salaam kuungua na kuteketea kabisa kwa moto.
Baba wa familia, Bwana Masoud Matal alisalimika kwa vile hakuwamo katika
nyumba hiyo wakati ikiungua.
“Nimepokea kwa
mshtuko mkubwa na nimesikitishwa mno kutokana na taarifa za kupoteza maisha kwa
watu tisa wa familia moja ya Bwana Masoud Matal baada ya nyumba yao kuunguzwa
na kuteketezwa kabisa na moto alfajiri ya tarehe 27 Agosti, 2015”, amesema kwa huzuni Rais Kikwete
akiomboleza vifo vya wanafamilia hao.
“Kwa hakika
hili ni pigo kubwa kwa Bwana Masoud Matal, lakini namuomba awe mvumilivu kwa
machungu yote ya kupotelewa ghafla na familia nzima, lakini yote amwachie Mwenyezi Mungu muweza wa yote”, ameongeza
kusema Rais Kikwete.
Katika salamu
zake hizo, Rais Kikwete amemwomba Mheshimiwa Sadik kumfikishia Salamu zake za
rambirambi na pole nyingi kwa Bwana Masoud Matal kutokana na msiba huo mkubwa uliompata,
na amesema anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema azipokee na kuzilaza
Mahala Pema Peponi Roho za Marehemu wote, Amina.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
28 Agosti,2015
via ikulu mawasiliano
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni