promotion

Jumamosi, 15 Agosti 2015

FAHAMU KUHUSU UVIMBE KWENYE OVARI KWA MWANAMKE

mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Leo ningependa nitoe utangulizi wa mada ambayo itakuwa ikiwekwa katika ukurasa huu kwa majuma kadhaa yajayo. Mada yenyewe inahusu tatizo la uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovari).Watu wengi wamekuwa wakisikia wengine yamewakuta na wengine hawajui lolote kuhusu tatizo hili. Niweke wazi kwamba katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kuna uvimbe mwingi ambao hutokea sehemu mbalimbali katika mfumo wao wa uzazi.
Kila sehemu ambayo uvimbe hutokea kuna sababu zake na dalili zake.Hivyo, ni vema unapofanyiwa uchunguzi hospitali ukaambiwa una uvimbe kwenye kizazi ni vema ukauliza uvimbe huo upo sehemu gani ili upate uelewa zaidi wa tatizo lako.
Kabla hatujaingia kwa undani kujadili tatizo hili ni vema tukapeana maelezo ya msingi ili kufahamu uvimbe huo hutokea sehemu gani, huitwaje na visababishi vyake.Uvimbe kwenye ovari hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke.
Ovari ni nini?
Kwa kawaida mwanamke anakuwa na ovari mbili katika mwili wake. Yaani moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto kwake. Ovari hizi hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (uterus).

Hakuna maoni: