mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Licha ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupiga vita kwa ukali suala la Rushwa ndani ya chama, hali inaonekana kwa wanachana wake hawako tayari kuachana a hali hiyo, baada ya jana kudhihirisha kuwa rushwa bado mchwa kwa taifa, baada ya mkutano mkuu wa chama hicho uliokuwa na lengo la kuwatafuta wagombea wa nafasi ya ubunge katika wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, kuvunjika kutokana na kubainika kuwepo kwa vitendo vya rushwa.
Mkutano huo ulivunjika majira ya saa 3:30 mchana, baada ya viongonzi wa chama hicho wilaya, pamoja na wasimamizi kubaini kuwepo kwa vitendo vya rushwa kwa wagombea kubainika wanagawa fedha kwa wajumbe ili wawapigie kura.
Kabla ya kutangazwa kuvunjika kwa mkutano huo vitendo vya rushwa vilianza kujitokeza mnamo saa 6:00, baada ya wapambe wa wagombea kuanza kugawa fedha kama njugu kwa wajumbe huku baadhi yao wakikamatwa na vijana wa ulinzi wa chama hicho (Red briged) baada ya kukutwa wakigawa fedha hizo.
Mtando wa Simiyu News ulishuhudia vijana hao wa ulinzi wakiwakamata akina mama wawili (majina yahifadhiwa) pamoja na mmoja wa mpambe wa mgombea Masunga Kiyumbi wakiwapeleka chumba maalumu katika ukumbi uliokuwa unatumika kufanyia mkutano huo kwa ajili ya mahojiano.
Mjadala ukiendelea nje ya ukumbi baada ya mkutano kuvunjika. |
Hata hivyo ilibainika kuwa baadahi ya wapambe wa wagombea walikutwa wakigawa fedha hizo kiasi cha shilingi 20,000 kwa kila mjumbe.
Mara baada ya kuhojiwa na vijana hao wa ulinzi, mpambe huyo alipotakiwa na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mkutano kujibu tuhuma zinzomkabili, alisema kuwa yeye alikuwa akitoa fedha kwa watu waliomuomba awanunulie maji ya kunywa.
“ ni kweli nimekamatwa na kuhojiwa lakini siyo rushwa..mimi watu mbalimbali wakiwemo wanawake..waliku wakiniomba niwanulie maji ya kunywa..na mimi sikukataa nikawa natoa pesa nfukoni kwa ajili ya kuwanunulia ndipo nikakamatwa” Alisema mpambe huyo.
Alibainisha kuwa kuwanunulia maji watu waliomuomba hiyo siyo rushwa bali ni upendo na kueleza kuwa yeye siyo mgombea bali alikuwa anaonyesha upendo kwao, ambapo aliwataka waandishi wa habari wasiandike habari hiyo kwani inamchafua yeye pamoja na mgombea wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni