mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Na samweli mwanga:
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo,Dr Titus Kamani amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutukanwa hadharani matusi ya nguoni na kutishiwa kupigwa na baadhi ya wananchi katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu kwa kile kilichoelezwa kutumia maneno ya kuudhi dhidi ya wananchi hao na Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki(CHADEMA) Slvester Kasulumbayi wakati wa sherehe hiyo ya kukabidhi matrekta hayo.
Matrekta kutoka Kiherya Invesiment Mwanza kupitia benki ya TIB.kabla ya kukabidhiwa kwa kituo cha nyalikungu saccos |
Na samweli mwanga:
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo,Dr Titus Kamani amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutukanwa hadharani matusi ya nguoni na kutishiwa kupigwa na baadhi ya wananchi katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu kwa kile kilichoelezwa kutumia maneno ya kuudhi dhidi ya wananchi hao na Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki(CHADEMA) Slvester Kasulumbayi wakati wa sherehe hiyo ya kukabidhi matrekta hayo.
Viongozi wa CCM waliokuwepo katika sherehe hiyo walitumia muda mwingi
kujinadi na kukipigia debe chama hicho na kugeuza kuwa jukwaa la siasa
huku Mbunge huyo akinyimwa nafasi hali iliyowakera baadhi ya wananchi
waliohudhuria sherehe hiyo.
Pia viongozi wa bodi ya Saccos hiyo walimulaumu Kamani kwa kukiuka utaratibu kwani alitakiwa ayakabidhi matrekta hayo kwa Nyalikungu Saccos na wao ndiyo wayakabidhi kwa wanachama waliopaswa kupewa baada ya kukidhi vigezo lakini alifanya kinyume hali ambayo ililalamikia na wajumbe hao akiwemo Mr Simba na Mohamed Macka.
Hali hiyo ilizua sintofahamu huku wananchi wakikumbwa na butwaa na kushindwa kujua kinachoendelea kulaumu kuchanganya sherehe hiyo na masuala ya Siasa.Kufuatia hali hiyo Waziri Kamani ilibidi aondoke katika eneo hilo kwani hali ilikuwa ni tete hata askari mgambo waliomwagwa eneo hilo ilionekana wazi wasingeweza kumudu vurugu hizo iwapo zingeendelea kuwa kubwa.
Hivyo viongozi hao wa kisiasa,Wasaccoss na wananchi kila mmoja alitaka kuongea na waandishi wa habari ambao walikuwa zaidi ya 15 katika sherehe hiyo.
Kasulumbayi alisema kuwa wamefanya hivyo kwa ajili ya kuona aibu hasa viongozi wa CCM Maswa ambao mwanzoni walizua maneno kuwa amechukua fedha za wananchi na kuwatapeli na hivyo Matrekta hayatafika.
Dr Kamani alidai kuwa ameamua kufanya hivyo alipata habari kuwa kuna baadhi ya wanasaccos wanataka kutapeliwa wasipewa matrekta alipobanwa kuelezwa na wakina nani hao waliotaka kutapeliwa na wengine wametapeliwa akashindwa kutoa jibu na kusisitiza ameagiza TAKUKURU wafuatilie suala hilo na kusisitiza kuwa serikali imeagiza kufanya hivyo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni