mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Alipotafutwa mganga mkuu wa wilaya hiyo Majeda
Kihulya alikataa kuongelea suala hilo, huku akieleza kuwa majibu ya vipimo
vilivyopelekwa Bugando yatakapoletwaa na Mkuu wa wilaya husika ndiye atakayetoa
katika vyombo vya habari.
Hali ya taharuki imewakumba wananchi katika wilaya
ya Meatu Mkoani Simiyu, baada ya kuibuka ugonjwa wa hajabu uliowakumba wananchi
hao ambao dalili zake ni kuongea ovyo, kuishiwa nguvu pamoja na kuumwa kichwa.
Bado haijajulikana ni aina gani ya ugonjwa
kutokana na baadhi ya waathirika waliofikishwa katika vituo vya afya kupimwa na
kubainika hawana ugonjwa wowote na badala yake kubaki wakiweweseka.
Akiongea na majira Mkuu wa wilaya hiyo Erasto Sima
alisema kuwa ugonjwa huo ulianza usiku wa kuamkia tarehe 02 mayi 2015, katika
kata za Mwandoya, Mwabusalu, Lingeka, Mwakisandu, Tindabuligi, Pamoja na
Lubiga.
Sima alieleza kuwa tangu kuibuka kwa ugonjwa huo
idadi ya wagonjwa imezidi kuongezeka kila siku, ambapo alibainisha kuwa mpaka
jana wamefikia jumla ya wagonjwa 80 kutoka katika kata hizo.
Aidha sima aliongeza kuwa timu ya wataalamu,
wahudumu wa afya, pamoja na madaktari kutoka katika hospitali ya wilaya hiyo,
tayari wamewasili katika kata hizo kwa kushirikina na wataalamu wa afya waliopo
ili kuongeza nguvu kutoa huduma ya kwanza.
Alisema kuwa wagonjwa mbalimbali ambao wamekuwa
wakiletwa wamekuwa wakionyesha dalili na kuishiwa nguvu, kuongea maneno
yasiyoeleweka, kuwapiga wenzio, kugongwa na kichwa, kutokwa na mafua, ikiwa
pamoja na kukohoa kikohozi kikavu.
Alieleza kuwa ofisi ya mganga mkuu wa mkoa
iliwasili baada ya kutokea kwa ugonjwa huo, ambapo sampuli zilichukuliwa kwa
ajili ya kupelekwa katika hospitali ya rufaa Bugando iliyoko Mkoani Mwanza kwa
ajili ya vipimo ili kubaini ni aina gani ya ugonjwa.
Alisema kuwa taarifa alizozipata ambazo hana
uhakika nazo kutokana na kutokudhibitishwa na wataalamu, kuwa ugonjwa huo
unaambukizwa na wanyama wa porini kwa kile alichoeleza baadhi ya waathirika wanapakana na pori tengefu la Maswa.
Hata hivyo aliongeza kuwa awali walipata taarifa
kutoka kwa wananchi kuwa kabla ya kutokea ugonjwa huo kwao mifugo ikiwemo
ngo’mbe ilikuwa ikishika na ugonjwa huo kwa kuweweseka hadi kupoteza uhai.
Aliongeza kuwa bado hawajatambua ugonjwa huo
unaambukizwa kwa hewa, au kushikana mikoni kwa kile alichoeleza bado
wanasubilia majibu ya vipimo vilivyochukuliwa katika hospitali ya rufaa bugando.
“ bado hatujatambua dalili zake ni nini?
Unaambukizwaje?.. kutokana na vipimo vilivyopelekwa vikiwa bado havijarejeshwa…lakini
huduma ya kwanza inaendelea kutolewa na tumeongeza nguvu za kutoa huduma hizo”
Alisema Sima.
Aliongeza kuwa ugonjwa huo unawashika watu wote
wakiwemo watoto, huku akieleza kuwa afisa mifugo na misitu ametumwa katika
ameneo hayo ili kuchunguza kama ugonjwa huo unasababishwa na wanyama kama
ilivyoelezwa na wananchi hao.
Kuhusu ugonjwa kuhusishwa na imani za kishirikina
mkuu huyo wa wilaya alikanusha habari hizo na kueleza kuwa hakuna dalili ambazo
zimeoneshwa kuwa ugonjwa huo unatokana na imani za ishirikina.
Aliongeza kuwa baadhi ya wagonjwa ambao wamefika
kupatiwa huduma kutokana na ugonjwa huo, walikutwa na magonjwa mengine
mbalimbali ukiwemo ugonjwa wa maralia ambao alisema walitibiwa na kupona hadi
kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni