Harlena Michelle Cooks alipokuwa akisukumwa na polisi hao (hawapo pichani) |
.
Video mpya imeenea mitandaoni ikiwaonesha Maofisa polisi wawili wa Kimarekani mjini Barstow huko California, Marekani wakimsukuma chini mwanamke mwenye ujauzito wa miezi 8 mwenye asili ya Kiafrika huku mikono yake ikiwa imefungwa kamba nyuma ya mgongo.
Tukio hilo linadaiwa kutokea hivi karibuni wakati polisi hao walipomtaka mama huyo aliyetambulika kwa jina la Harlena Michelle Cooks awaoneshe kitambulisho chake na yeye kukataa kuwaonesha ndipo walipochukua jukumu la kumsukuma kutoka kwenye gari mpaka chini jambo ambalo liliamsha hasira kwa raia wengi wa Marekani weusi (wenye asili ya Kiafrika) na kufanya manadamano katika mji wa California.
Video hiyo iliyotolewa na Shirika la haki za binadamu la American Civil Liberties Union Foundation (ACLUF) imeenea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kupokelewa kwa hisia kali na Wamarekani weusi pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu.
Kitendo hicho kimejadiliwa kuwa ni cha kibaguzi, kikatili, kiunyanyasaji na kinakiuka haki za binadamu.
Tukio hilo limejiri huku kukishuhudiwa ongezeko la vitendo vya udhalilishaji na ukatili vya polisi weupe dhidi ya Wamarekani weusi.
Tayari vijana kadhaa wa Marekani wenye asili ya Afrika wameuawa bila hatia mikononi mwa polisi weupe mwaka huu, suala linaloonyesha kuendelea ubaguzi wa rangi katika nchi ambayo inajigamba kuwa na eti rekodi nzuri ya uadilifu na usawa kwa watu wote.
CHANZO: IRANSWAHILI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni