promotion

Jumanne, 19 Mei 2015

MWIMBAJI WA ‘KUCHI KUCHI’ ATOA SABABU YA UKIMYA WAKE

mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Mwimbaji wa kike wa Nigeria, J’Ordie.

MWIMBAJI wa kike wa Nigeria, J’Ordie alipotoa wimbo wa ‘Kuchi Kuchi’ ambao unafanana na nyimbo za Kihindi, wapenda burdani wengi nchini humo walijua wamepata staili mpya ya nyimbo katika tasnia hiyo, lakini wakati wakifikiri kwamba mwimbaji huyo angezidi kutoa nyimbo nyingine, alipotelea katika ukimya.
Wakati mashabiki wakijiuliza kilichotokea, mwimbaji huyo mrembo alizungumza na gazeti la Daily Independent akisema katika sanaa inafaa kujipanga vizuri zaidi ili kuweza kutoa kitu kizuri kwa mashabiki.
“Sifa zinahitaji matayarisho na si kukurupuka tu.  Isitoshe, kwa msanii kuhakikisha anabaki katika tasnia ya burudani bila kutetereka hivi sasa ni vigumu kuliko ilivyokuwa hapo nyuma,” alisema J’Ordie.

Hakuna maoni: