mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Afisa habari wa jeshi la polisi Mkoani Simiyu Mudi Ramadhan, akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) baadhi ya viuongo vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu ambavyo vimekamatwa na jeshi hilo |
Jeshi la
polisi Mkoani Simiyu linamshikilia Chigila Gilala mkazi wa kijiji cha Bukigi
kata ya Malampaka wilayani Maswa (45) kwa kosa la kukutwa na viungo
zinavyozaniwa kuwa vya binadamu likiwemo fuvu la kichwa.
Mtuhumiwa huyo
ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM katika kijiji hicho na Mganga wa tiba asili alikamatwa
nyumbani kwake, baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa alikuwa amewahifadhi majambazi kwa ajili
kugangwa (kuzindikwa).
Akitoa taarifa kwa waandishi wa kamanda wa jeshi la polisi Mkoani hapa Gemini Mushy
alieleza kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa mwenyekiti huyo lilitokea may 9 mwaka
huu majira ya saa 11 jioni katika kijiji
hicho.
Kamanda
Mushy alisema kuwa askari wakiongozwa na mkuu wa upelelezi katika wilaya ya
maswa walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwepo kwa majambazi nyumbani kwa
mganga huyo, kuwa alikuwa amewahifadhi kwa ajili ya kuwazindika.
Viungo vya Binadamu vilivyokamatwa, fuvu la kichwa pamoja na mifupa ya mikono au miguu. |
Alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo walifanya msako nyumbani kwa mwenyekiti huyo,
ambapo alibainisha kuwa walianza kufanya
upekuzi ndani na nje ya nyumba.
“ wakati
wakifanya upekuzi huo walikutana na mfuko wa sandaruzi ukiwa chini ya lundo la
kuni nje ya nyumba ya mwenyekiti
huyo..na katika mfuko huo kulipatikana fuvu la kichwa pamoja na mifupa ya
mikono au miguu vinavyodhaniwa kuwa ni viungo vya binadamu” Alisema Mushy.
Kamanda alieleza
kuwa jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi kama kweli viungo hivyo ni vya binadamu
na kama anahusika na uwepo wa viungo hivyo kutokana na kukutwa nje ya nyumba yake.
Wakati huo
huo kamanda Mushy alibainisha kuwa jeshi hilo linamshikiria Gandula Mashimo mkazi wa kijiji cha
Longalombogo kata ya Migato wilaya ya
Itilima Mkoani hapa kwa kukutwa na
Bunduki ya kivita SMG na risasi 273.
Alisema kuwa
mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi majira ya saa 3:30 usiku kijijini hapo, akiwa
embeba siraha hiyo pamoja na risasi katika mfuko wa sandarusi.
Alisema kuwa
mtuhumiwa alikamatwa baada ya wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi wilayani
humo, ambapo alikamtwa akiwa njiani kuelekea kusikojulikana.
Mushy
alieleza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini washirika wake, ikiwemo na
matumizi ya silaha hiyo, huku akitoa wito kwa wananchi mkoani hapa kutoa
taarifa za watu wanaowahisi kuwa siyo wema katika maeneo yao.
Aidha alitoa
onyo kwa ambaye anamiliki silaha bila kibali rasmi, kuwa ajisalimishe pamoja na
silaha yake mara moja kabla ya msako mkali kuanza.
Risasi zikiwa jumla 273 |
Kamanda wa polisi
Mkoa Polisi Mkoa wa Simiyu Gemuni Mushy akiwaonyesha waandishi wa
habari (hawapo pichani) Bunduki aina ya SMG ya kivita ambayo imekamatwa
na jeshi hilo. SOURCE SIMIYU NEWS |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni