Moja ya nchi zenye kiasi kikubwa cha joto duniani ni pamoja na India ambayo unaambiwa kwa sasa joto lake linafikia nyuzijoto 48 katika maeneo mengi.
Taarifa ambayo si nzuri kutoka nchini humo zinasema watu wapatao 500 wamepoteza maisha kufuatia kuongezeka kwa joto huku idara ya utabiri wa hali ya hewa ikisema hali hiyo ya juu ya joto inatokana na kukosekana kwa mvua kwa muda mrefu.
Maafisa utawala wameanza kampeni ya kuwahamasisha wananchi kukaa majumbani mwao na kuwashauri wanywe waji mengi.
Majimbo yaliyoathirika ni pamoja na Andra Pradesh ambalo ndilo lililoongoza kwa kupoteza idadi kubwa ya watu waliofikia 246.
Vifo vingi zaidi vimeripotiwa katika majimbo ya kusini ya Telangana na Andhra Pradesh, ambapo watu 140 wamepoteza maisha yao kuanzia siku ya jumamosi hadi leo wakati wimbi hilo la joto lilipotokea.
Mji wa Allahabad ulioko Uttar Pradesh ulisajili vipimo vya nyuzijoto 48C huku wakazi wa mji mkuu wa India, New Delhi ukiwa na kiwango cha nyuzijoto 44C .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni