Maelfu
ya wakimbizi kutoka Bangladeshi na Myanmar wametelekezwa karibu na ufuo
wa Thailand kufuatia masharti makali yaliyowekwa majuzi.
Shirika
la kimataifa linalishoghulikia maswala ya wahamiaji IOM, limesema kuwa
hatua ya hivi punde ya serikali kuvunjilia mbali kambi za wakimbizi na kuwakamata
maharamia wanaolangua watu imewaogopesha wakimbizi hao wanaotoroka
mateso katika mataifa hayo kushindwa kufika ufukweni. Msemaji wa
shirika hilo ameiambia BBC kuwa watu hao wa tabaka la Rohingya
wameshindwa kuingia Thailand na hivyo kusalia wakielea baharini wasijue
cha kufanya. Hata hivyo polisi nchini humo wanasema kuwa zaidi
ya wakimbizi haramu elfu moja waliwasili nchini humo katika kipindi cha
siku chache zilizopita. Aidha Polisi wanadai kuwa wakimbizi hao waliwasili kupitia ufukwe wa Langkawi ulioko Kaskazini Mashariki mwa kisiwa hicho.
Mapema leo duru za polisi
zimedokeza kuwa wakimbizi wengine elfu moja wamewasili Aceh
wakishukiwa kuwa ni sehemu ya jamii ya Rohingyas wanaotoroka mateso
kwao. Wakimbizi wengine 600 ambao pia wanaaminiwa kutoka jamii ya Rohingya walishekwa na utawala wa indonesia siku ya jumapili. Serikali
ya Thailand iliamua kukaza kamba na kutangaza vita dhidi ya makundi
yanayowalangua wanadamu baada ya kugundua makaburi thelathini ya karibu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni