mcharoman blogy fahar yako mtanzania
DIAMOND NA HAWA KWENYE VIDEO YA NITAREJEA |
Kauli yake Kuu HAWA:NITAREJEA NI “WIMBO NINAOUCHUKIA SANA.ULINIHARIBIA MAISHA YANGU”.
Kama wewe ni mmoja wa Wapenzi wa msanii Diamond na Mpenzi wa Wimbo wake Uleee uitwa NITAREJEA Basi kuna kitu unatakiwa Kukijua hapa.
MWANADADA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA HAWA ALIYETAMBA NA KUFANYA VIZURI KATIKA WIMBO WA NITAREJEA WA MSANII DIAMOND PLATNUM AMBAYE NI HABARI YA MJINI NDANI NA HATA NJE YA NCHI AMESEMA MAISHA YAKE NI MAGUMU KUPITA KIASI KUTOKANA NA DIAMOND KUSHINDWA KUMPA MSAADA LICHA YA WIMBO ULE KUFANYA VIZURI SOKONI.
HAWA AMESEMA HAYO AKIZUNGUMZA KATIKA KIPINDI CHA BURUDANI KINACHORUSHWA NA KITUO CHA MLIMANI TV YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM AMBAPO AMESEMA LICHA YA COLLABO YAKE NA DIAMOND KUWA CHANZO CHA UMAARUFU WAKE LAKINI MATOKEO YAKE AMEISHIA KUJUTA NA KUTOAMBULIA CHOCHOTE.
HAWA AMEKIRI KUWA NITAREJEA NI WIMBO ANAOUCHUKIA MILELE KATIKA MAISHA YAKE KUTOKANA NA KILE UNACHOMKUMBUSHA KILA ANAPOUSIKIA.
ALIPOULIZWA KAMA ANAMCHUKIA DIAMOND.HAWA AMESEMA HANA CHUKI NA DIAMOND LAKINI AMEMTAKA STAR HUYO KUKUMBUKA ALIPOTOKA.
‘’MIMI NAMWAMBIA ARUDI KIJIJINI’’ALISEMA HAWA ALIPOULIZWA KIPI ANACHO KUMWAMBIA DIAMOND .
MWANADADA HUYO PIA AMETOA WIMBO WAKE MPYA NA VIDEO AMBAYO ITATAMBULISHWA HIVI KARIBUNI AKIELEZEA MAISHA YAKE ZIKIWEMO SHIDA ALIZOPITIA.
NA PIA ANA WIMBO MWINGINE AMBAO UNAELEZEA KISA CHAKE NA DIAMOND KIKIWA KAMA MWENDELEZO WA WIMBO WA NITAREJEA.
HATA HIVYO AMEKANUSHA TUHUMA ZILIZOZUKA ZA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA LAKINI AKAKIRI KUWA BAADA YA KUCHANGANYIKIWA BAADA YA KUPEWA UJAUZITO NA MWANAUME ALIYEAHIDI KUMSAIDIA KIMUZIKI(SIYO DIAMOND) ALIANZA KUNYWA POMBE KUPITILIZA NA HATA ALIPOMTAFUTA DIAMOND MARA NYINGI KUTAKA MSAADA WAKE DIAMOND ALIKATAA KUMPA USHIRIKIANO.
KWA MUJIBU WA HAWA ALIKUTANA NA DIAMOND WAKATI AKIWA THT NA ALIPOMSIKIA AKIIMBA ALIKUBALI KIPAJI CHAKE NA AKAMUOMBA WAFANYE WIMBO KWA PAMOJA NA MPAKA LEO HAJAWAHI KUPATA HATA SHILINGI MOJA YA DIAMOND KUTOKA KATIKA WIMBO ULE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni