mcharoman blogy fahar yako mtanzania
MUME wa ‘long time’ wa mwimbaji nyota wa kike wa muziki wa Taarab nchini, lsha Ramadhan ‘Mashauzi’, Jumanne Hassan ‘Tevez’ ambaye hivi karibuni alitekwa na kuteswa na watu wasiofahamika nchini Afrika Kusini, amerejea nchini na kufanya dua ya kumshukuru Mungu kwa kumnusuru kifo katika tukio hilo.
Tevez aliwakusanya ndugu, jamaa na marafiki na kufanya dua hiyo, Ijumaa iliyopita nyumbani kwao Msamvu, Madawa jirani na Shule ya Msingi Msamvu ‘A’ ambapo alifanya kisomo hicho kilichoambatana na dua na chakula.
“Mungu amemnusuru na balaa lile, amemkingia hivyo ameona ni vyema aandae dua ya kumshukuru,” alisikika mmoja wa waalikwa.Baadhi ya mashehe na waumini wengine wa Kiislamu waliohudhuria dua hiyo walimpongeza Tevez kwa kitendo hicho cha kumkumbuka Mungu na kumshukuru kwa kumlinda na majanga yaliyomkuta.Watu waliohudhulia dua hiyo.
“Hili ni jambo jema sana alilofanya Tevez ambapo tunaelekezwa na mitume wetu kwamba tumshukuru Mungu kwa kila jambo,” alisema mmoja wa waumini wa dini ya Kiislamu.Kwa upande wake Tevez alisema amamshukuru Mungu kwani amempigania sana uhai wake.
“Lilikuwa ni tukio kubwa kwangu, sikutegemea kama ningenusurika, Mungu amenipigania sana nimeona bora nijumuike na ndugu, jamaa na marafiki kumshukuru Mungu,” alisikika Tevez.Januari mwaka huu, Tevez alitekwa na watu wasiojulikana katika mji wa Durban nchini Afrika Kusini ambapo mwenyewe alibainisha kuwa mwenyeji wake mjini humo alivujisha habari kuwa ana fedha ndipo akavamiwa, akateswa na kuporwa fedha na simu zake mbili.Majeraha ya mgongoni aliyoyapata wakati akiwa Sauz.
Tevez aliwafungulia mashtaka vijana waliohusika na tukio hilo ambapo kesi inaendelea kuunguruma nchini humo.
STORY BY GLOBAL PUBLISHER
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni