promotion

Jumanne, 7 Aprili 2015

SIKU ZA HATARI ZA KUSHIKA MIMBA NI ZIPI?

mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Habari za wakati huu wapendwa wafuatiliaji wa blog hii! kabla ya kuanza mada hii ya leo napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu kuweza kuniweka hadi hivi sasa nikiwa na afya njema

Mada yangu leo inahusu siku za hatari ambazo mwanamke  akifanya ngono bila kinga basi anakuwa katika hatari ya kushika mimba.

Nimeamua kutoa mada hii baada ya kugundua kuwa ongezeko la matukio ya utoaji mimba, utupaji wa watoto  na hata kuwa na watoto wa mitaani yanasababishwa  zaidi na mimba ambazo hazikutarajiwa ambazo zingine zinatokana na mzazi kutokujua siku yake ya hatari ili kujikinga.

Ni muhimu sana kwa mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, mizunguko hiyo iko katika makundi makuu matatu3 ambayo ni : mzunguko mfupi(siku25 kurudi nyuma), mzunguko wa kawaida(siku28) na mzunguko mrefu(siku30-35)

 Wanawake wengi mzunguko wao  huwa  ni wa kawaida yaani siku 28 hawa ndio leo nitawaongelea zaidi.

 NAMNA YA KUTAMBUA MZUNGUKO WAKO.

Ili kutambua mzunguko wako ni wa siku ngapi unatakiwa kuhesabu kuanzia siku ya kwanza kuona damu ya hedhi hadi siku ya kwanza ya kuona damu ya hedhi ya mwezi unaofuata, kwa mfano ukiona damu ya hedhi tarehe 15 December basi hiyo ndio siku yako ya kwanza.

Kwa mtu mwenye mzunguko huo wa siku 28 siku zake za hatari za kuweza kushika mimba ni siku ya kumi na nne 14, hivyo kuanzia siku ya 12 hadi siku ya 16 kama atafanya ngono bila kinga anaweza kushika mimba.

Najua mtu anaweza akajiuliza kama siku ya hatari ni ya 14 sasa kwa nini akifanya ngono siku ya 12 anaweza akapata mimba?
Hii ni kwa sababu mbegu za kiume zina uwezo wa kudumu kwa masaa24 hadi 48 baada ya kujamiiana hivyo kama utafanya ngono tarehe 12 na yai likatoka tarehe14 bado litakuta zile mbegu zikiwa hai hivyo zitarutubishwa.

kwa leo tuishie hapo mpendwa mfuatiliaji ili kukuachia nafasi ya kuchangia zaidi na kuboresha yale ambayo sikuweza kuelezea hapo.

pia ninakaribisha maoni juu ya Afya ya uzazi, vyakula bora kwa afya, na maswala ya VVU na Ukimwi.



Hakuna maoni: