promotion

Jumatano, 8 Aprili 2015

SAKATA LA MGOMO WA MADEREVA NCHI NZIMA KUJULIKANA IJUMAA HII

mcharoman blogy fahar yako mtanzania

KUFUATIA serikali kushindwa kufuatilia na kutatua kero na matatizo yanayowasibu madereva wa magari na pikipiki hapa nchini, Muungano wa Vyama cha Madereva nchini umepanga kugoma kuingia barabarani kutoa huduma ya usafirishaji nchi nzima ili kuishinikiza serikali kusikiliza na kutatua kero zinazowasumbua kwa miaka mingi sasa.
Wakizungumza na vyombo vya habari kupitia Katibu wa Muungano wa Vyama vya Madereva, Bw. Rashid Saleh, madereva hao wamesema kuwa suala la kurudia kusoma kila wanapohuisha leseni zao ni aina nyingine ya unyanyasaji kwa maelfu ya madereva nchini, ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa hawana mfumo mzuri wa ajira licha ya kutupiwa lawama nyingi na serikali na wadau wengine wa usafiri kuwa wao ndio chanzo cha ongezeko la ajali hapa nchini.


Katibu huyo wa Muungano wa Vyama vya Madereva ameitaja kero nyingine kuwa ni hatua ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (National Institute of Transport NIT) kutamka hadharani kuwa vyeti walivyonavyo madereva hao sio halali na kwamba Ijumaa wiki hii wanakusudia kukutana na Waziri wa Kazi na Ajira kwa ajili ya kuzungumzia kero hizo kwa lengo la kuepusha kutokea kwa mgomo huo.
Bw. Saleh ametaja madereva wanaounda muungano huo kuwa ni wa bodaboda, bajaj, teksi, daladala, mabasi ya safari fupi, mabasi ya safari ndefu na za nje ya nchi pamoja na madereva wa magari yote ya mizigo.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa Muungano wa Madereva nchini, mkutano wa Ijumaa ndio utakaoamua iwapo madereva hao wagome au waendelee na kazi kwani wamechoka kudharauliwa hata kwa mambo ya msingi yanayogusa maisha yao.
Baadhi ya dharau alizozitaja ni pamoja na wamiliki wa mabasi (yaani waajiri wao) kuwaita wao ni wahuni ilhali ni watu wazima, wenye familia, wanaofanya kazi halali na wanaohitaji kuheshimiwa.
Jambo lingine lililozungumzwa na umoja huo ni kuhusu Mamlaka ya Usafirishaji wa Majiini na Nchi kavu SUMATRA kushindwa kutangaza viwango vipya vya nauli kama ilivyoagizwa.

Hakuna maoni: