promotion

Alhamisi, 23 Aprili 2015

RISASI YALIA BAADA YA CHENGE KUKUTANA USO KWA USO NA WAFUASI WA CHADEMA WILAYANI BARIADI MKOANI SIMIYU

mcharoman blogy fahar yako mtanzania

Katika hali isiyo ya kuwa yakawaida jana Mbunge wa Bariadi Mgaharibi Edrew (CCM) Chenge amenusurika kipigo kutoka kwa wafuasi wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Simiyu baada ya kupita katika ofisi zao akitoka kwenye mkutano wake.

Hali hiyo ilitokea baada ya wafuasi wa chama hicho kuzuia msafara wa Mbunge  huyo na kuanza kurushia mawe magari yalikuwa katika masafara huo ambapo mmoja wa makada wake alijulikana kwa jina la Ahmed Ismail alilazimika kurusha risasi tatu hewani ili kuwatanya watu waliokuwa wameziba njia.

Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa moja na nusu usiku baada ya vyama hivyo  CCM na Chadema kumaliza mikutano yao ya hadhara iliyokuwa ikifanyika katika maeneo tofauti mjini Bariadi hali ambayo ilisababisha kuwepo kwa vuugu hizo.

Hali hiyo imetokea baada ya msafara wa Chenge kuondoka katika mkutano wao uliokuwa katika kijiji cha Isanga jimboni kwake, ambapo wakati wakipita katika ofisi za Chadema Mkoa zilizoko barabara kuu ya Bariadi-Shinyanga walianza kuzomewa na wafuasi wa chama hicho.


Akidhibitisha kuwepo kwa tukio hilo Kamishena Msaidizi wa jeshi la polisi Mkoani hapa Gemini Mushi alisema kuwa vyama hivyo baada ya kumaliza mikutano yao Chadema walianza safari ya kuelekea katika ofisi zao huku msafara wa  ulikuwa ukirejea .

Kamanda alibainisha kuwa Baada ya msafara huo kufika katika eneo la ofisi ya chadema walikuta kundi kubwa la watu wakishangilia na ndipo mbunge huyo akashuka kwenye gari na kuanza kuchenza nao wakati wakiendelea kushangilia walisikia sauti ikisema rusha mawe hali ambayo ilisababisha mbunge huyo kukimbilia kwenye gari.

Mushi alisema kuwa baada ya wafuasi hao wa chadema kurusha mawe wakishambulia gari alilokuwa amepanda mbunge huyo ndipo risasi tatu zilirushwa hewani kwa ajili ya kuwatawanya na kufanikisha wafuasi hao kukimbia na ktawanyika.
Mushi alieleza kuwa baada ya tukio hilo wafuasi wote wa vyama viwili walikimbilia kituo cha polisi Bariadi kutoa taarifa, ndipo askari wake walifika eneo la tukio na kuanza uchunguzi.

Alisema risasi hizo zilizorushwa na mfuasi huyo wa Chenge zilikuwa na lengo la kuwatawanya wafuasi hao ambao alisema walianza kuleta vurugu, huku akieleza kuwa siraha hiyo ni bunduki aina ya bastola.

Kamanda huyo alieleza kuwa uchunguzi bado unaendelea kufanyika ili kubaini chanzo cha vurugu hizo, huku akieleza kuwa hakuna mareruhi na hakuna mtu anayeshikiliwa na jeshi hilo.

Mashududawa tukio hilo

Baadhi ya mashuda wa tukio hilo wameeleza kuwa baada ya kukutana hapo wafuasi wa vyama hivyo waliaza kurushiana mawe na ndipo mbunge kukimbilia kwenye gari na baadhi ya wafuasi wa chadema walianza kuirushia mawe gari aliyokuwa amepada mbunge hali ambayo iliwalazimu kurusha risasi mmoja wa makada wa ccm waliokuwa katika gari hilo.

“tulishangaa kuona wafuasi wa ccm na chadema kuanza kushambuliana kwa mawe baada ya watu wa ccm wakitokea katika mikutano yao ya hadhara na kufika katika maeneo ya salunda wafuasi wa ccm na chadema walikutana na kuanza kushambuliana kwa mawe baadaye tulisikia risasi zinalia”Alisema mkuba majaliwa shuhudawa tukiohilo.

Heche asimulia.

Kiongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema John Heche alisema kuwa chama cha CCM walipata katika ofisi za chadema wakakuta viongozi wanafanya mikutano ya ndani ambapo msafara wa CCM ulifika katika ofisi hiyo na kuanza kupiga miziki hali ambayo ilipelekea baadhi ya viongozi kutoka kwenda kuwazuia kwa madai ya kupunguza mziki.

“msafara wa ccm ulifika katika ofisi ya chadema baada ya kutoka katika mikutano yao walipofika katika maeneo ya ofisi zetu walisimamisha magari yao na kuanza kupiga mziki na wafuasi wao walitelemka kwenye magari na kuanza kucheza hali ambayo tulienda kuwazuia kwa misingi ya kupunza mziki kwani tulikuwa tunafanya kikao cha chama lakini walikaidi na ndipo wafuasi wetu walianza kuwashambulia kwa mawe hali ambAyo walirusha risasi hewani kwa ajili ya kutawanya”Alisema Heche.

Kwa upande wake katibu wa umoja wa vijana wa CCM wilaya ya Bariadi Sai Samba alieleza kuwa baada ya kufika katika eneo la ofisi ya Chadema walikuta kundi kubwa la vijana wakiwa barabarani ambapo walipofika wakazuia msafara na ndipo kundi la vijana walianza kumrushia mawe mbunge wao. Alisema baada ya kuona hali hiyo mmoja wa makada wao aliamua kurusha risasi hewani ili wafuasi hao wasimdhulu Mbunge huyo ambaye gari lake lilikuwa likishambuliwa kwa mawe.

 “baada ya kufika katika maeneo ya ofisi ya chadema tulikuta watu       ambao walikuwa wamejiandaa kwa ajili ya kuushambulia msafara wa mbunge Andrew Chenge na tulipofika pale walianza kucheza na mbunge akatelemka kwenye gari na kuanza kucheza nao lakini ilisikika sauti ikamuru vijana kurusha mawe na ndipo walianza kurusha mawe hali iliyopelekea kurusha risasi hewani”Alisema Samba

Walipotafutwa kuongelea suala hilo la kurusha risasi hewani Mbunge wa Bariadi Magharibi na kada huyo wa CCM Ahmed Ismail hawakupokea simu

Hakuna maoni: