Kiongozi wa Kanisa la Efatha, Nabii na Mtume Josephat Mwingira (pichani) ametema cheche kwamba wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia nafasi ya urais na ubunge wanaotumia ushirikina kuwania nafasi hizo, watakumbwa na mauti kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.
Mtume Josephat Mwingira
Mtume Josephat Mwingira
Akizungumza na waumini wa kanisa lake katika ibada maalum ya kuwekwa wakfu kwa jengo la Kanisa la Efatha lililopo Vwawa, Mbozi mkoani Mbeya, Mwingira alisema wote wanaotumia nguvu za giza kusaka madaraka, mwisho…
Kiongozi wa Kanisa la Efatha, Nabii na Mtume Josephat Mwingira (pichani) ametema cheche kwamba wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia nafasi ya urais na ubunge wanaotumia ushirikina kuwania nafasi hizo, watakumbwa na mauti kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.
Akizungumza na waumini wa kanisa lake katika ibada maalum ya kuwekwa wakfu kwa jengo la Kanisa la Efatha lililopo Vwawa, Mbozi mkoani Mbeya, Mwingira alisema wote wanaotumia nguvu za giza kusaka madaraka, mwisho wao ni kupoteza maisha katika vifo vya ghafla na kuwatahadharisha wananchi kuwa makini na watu wa namna hiyo.
“Mgombea atakayejihusisha na vitendo vya kishirikina hatachaguliwa na huyo atakufa kabla ya uchaguzi wenyewe maana Mungu anachukizwa sana na vitendo hivyo,” alisema Mwingira huku akishangiliwa na waumini wake.
Pia Mwingira aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura ili waweze kushiriki kupiga kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa na kuwachagua viongozi waadilifu.

Hata hivyo, Mwingira alisema kwamba hawezi kuwaelekeza waumini wake wapige kura ya ndiyo au hapana kwenye mchakato wa kupiga kura ya maoni isipokuwa waumini wenyewe ndiyo watakaoamua wanachoona kinafaa kwao.
Kauli hiyo ya Mwingira, imekuja siku chache tangu serikali kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe kuwaonya viongozi wa dini kuzungumzia siasa wawapo kwenye nyumba zao za ibada na kutishia kuzifuta taasisi zote zitakazobainika kukiuka maagizo hayo na zile ambazo zinafanya kazi tofauti na usajili wao.
Waziri Chikawe, alitangaza pia kuanzia Jumatatu ya wiki hii, serikali itaanza kuzipitia taasisi zote za kidini kwa ajili ya ukaguzi na kuzifunga zile zitakazobainika kukiuka baadhi ya vipengele muhimu, zikiwemo zinazohubiri masuala ya siasa kwenye nyumba za ibada
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni