mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Mahakama ya wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu imehairisha kesi inayomkabili Hakimu wa mahakama ya mwanzo Somanda wilayani hapa Janeth Mazigi (28) hadi tarehe 04 mayi mwaka huu kutokana na kuwa katika likizo ya uzazi.
Kesi hiyo ambayo imetajwa kwa mara pili chini ya Hakimu wa Mkazi wa mahakama hiyo Robert Oguda, wakili wa Mfawidhi wa serikali Mkoani hapa Yamiko Mlekano alieleza mahakama kuwa uchunguzi juu ya kesi hiyo umekamilika.
Wakili huyo aliiomba mahakama kutoa tarehe ya kuweza kusikilizwa kesi hiyo kwa mara kwanza, kwa madai kuwa mshitakiwa namba moja Mazigi yuko katika likizo fupi ya uzazi hivyo hakuweza kuhudhulia mahakamani.
Awali wakili huyo akisoma mashitaka yanayomkabili hakimu huyo alisema kuwa Mshitakiwa
inadaiwa kuwa alitumia wadhifa alionao kumteka mtumishi wa halmashauri ya mji ya Bariadi (jina linahifadhiwa) na kumnyanyasa kijinsia kinyume na sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16.
Mlekano aliieleza mahakama kuwa mnamo tarehe 3/03/2015 mshtakiwa pamoja na askati polisi wa kike walimteka Mtumishi huyo ofisini kwake kinyume na matakwa yake na kumpeleka nyumbani kwa mshitakiwa Kidinda Bariadi Mjini kinyume na kifungu namba 133 cha kanuni ya adhabu sura ya 16.
Kosa la pili la unyanyasaji wa kijinsia , ilidaiwa kuwa katika tarehe hiyo hiyo majira ya saa 3 hasubuhi nyumbani kwa Mshtakiwa , alimpiga picha za utupu mtumishi huyo kwa kutumia simu yake kwa lengo la kumdhalilisha na kumtolea maneno ya kashfa.
Kosa la tatu kukutwa na picha za uzalilishaji mshitakiwa ilidaiwa terehe hiyo hiyo majira ya saa 3 hasubuhi nyumbani kwa mshitakiwa alikutwa na picha za utupu zilizokuwa katika simu yake alizokuwa amempiga mtumishi huyo akiwa uchi kwa lengo za kuzituma katika mitandao ya kijamii ili kumdhalilisha kinyume na sheria na kanuni ya adhabu.
Kosa la nne ambalo ni wizi ilidaiwa mshitakiwa alimnyanganya Mtumishi huyo kiasi cha pesa taslimu Tsh 50,000, power bank, chaji, airphone, simu mbili za aina ya Son na Tecno vyote hivyo vikiwa na thamani ya Sh Mil 1,405,000.
Hata hivyo hakimu Oguda alikubali ombi la wakili huyo, na kesi kuhairishwa mpaka tarehe 04/5/2015.
Wakati huo huo mahakama hiyo imeharisha kesi inayowakabili askari wawili wa jeshi la magereza na polisi kwa kosa la kukutwa na noti bandia ikiwa pamoja na sare za jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ).
kwa mujibu wa wakili wa serikali mfawidhi Mkoani hapa Yamiko Mlekano alieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, lakini bado wanasubilia majibu kutoka Benki kuu ya Tanzania kuidhinisha kuwa ni noti bandia.
Kutokana na hali hiyo wakili huyo aliiomba mahakama kutoa tarehe nyingine ili kusikilizwa kwa kesi hiyo baada ya majibu kutoka benki kuu ya Tanzania kuwasili.
Hakimu makazi wa mahakama hiyo Robert Oguda alikubali ombi la wakili huyo, ambapo alihalisha kesi hiyo hadi tarehe 08/04/2015.
Askari hao ambao ni H 2420 PC Seleman Juma (25) ambaye ni askari wa kikosi cha kutuliza gasia FFU Mkoani Simiyu, na askari namba B.6499 WDR Edmund Masaga (28) ambaye ni askari Magereza wilayani Bariadi walikamatwa machi 22 mwaka huu majira ya saa 9 mchana katika mtaa wa Old Maswa kata ya nyakabindi Wilayani Bariadi wakiwa na noti bandia kama zilikuwa halali zingelikuwa na thamani ya Shilingi 1, 920,000.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni