Msanii Shaaban Seif ‘Shebbylove’ akiwa katika pozi.
WASANII wanatamba na wimbo wa Baikoko, Aboubakar Athuman ‘Beckatittle’ na Shaaban Seif ‘Shebbylove’ wamefunguka kuwa wanajivunia kuona staa mkongwe kama Ali Kiba ametambua uwezo wa prodyuza wao, Abydady wa Chiders Records na kufanya naye kazi.
Akizungumza Shebbylove alisema, wao waliutambua uwezo wa Abydady ndiyo maana walifanya naye kazi na bahati nzuri ngoma yao inabamba katika vituo mbalimbali vya redio pamoja na televisheni.
“Sisi ngoma yetu ni ya mfumo wa Baikoko tuliifanya kwa Abydady, Desemba, mwaka jana, Februari , mwaka huu akafuata Kassim Mganga na kupiga muziki kama wetu na sasa Kiba naye kakubali uwezo wa prodyuza wetu naye akarekodi ngoma yake mpya ya Chekecha, tunajivunia hilo,” alisema Sebbylove.