AFISA ARDHI WA WILAYA YA MASWA VIVIAN MKAMBA AKIZUNGUMZA NA WANAKIJIJI WA KIJIJI CHA SHISHIYU WILAYA YA MASWA.
|
Akizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Shishiyu, Kata ya Shishiyu Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu,
Afisa aridhi wa Wilaya hiyo, Vivian Mkamba alisema kuwa wabunge na madiwani
wanaweza kusaidia kupunguza migogoro ya aridhi vijijini kama watawahamaisha wananchi
kupima maeneo yao.
Mkamba alisema
kama wananchi wanaoishi vijijini wanataka kumiliki aridhi yao kwa amani ni
vyema wakajitokeza kupima mashamba yao ili wapate hati miliki za kimila ambazo
zimeanza kutolewa wilayani humo.
“Kumekuwa na
migogoro mingi ya aridhi hasa vijijini, lakini kwa sasa kuna hati miliki za
kimila ambazo zinatolewa vijijini, hivyo wananchi msione tabu kuchangia fedha
ilimpimiwe mashamba yenu na kuepuka migogoro isiyokuwa na tija, kwani kwa sasa
idadi kubwa ya wananchi wanaporwa maeneo yao kwa kukosa hati miliki,”alisema
Mkamba na kuongeza:
“Haya yanaweza
kufanyika kama wabunge na madiwani watasaidia kuwahamasisha wananchi kujitokeza
kupima maeneo yao, kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kupunguza migogoro ya aridhi
kati yao na wawekezaji.”
Akizungumza wakati
wa utoaji wa hati hizo kwa wananchi wa
kijiji cha Shishiu Kata ya Shishiu, Afisa kutoka
Shirika la Kibinadamu la Kimataifa la Oxfam Tanzania, Haji Kihwele
alisema kwa kutambua umuhimu wa wananchi
kumiliki aridhi wamekuwa wakishiriki kuhamasiha wananchi kujitokeza
mupimiwa maeneo yao iliwaweze kufanya shughuli zao ikiwemo kilimo bila usumbufu.
“Kuna wananchi
wanamiliki mashamba makubwa mengine yanafikia hadi hekari 500 na wengi
wanayatumia katika kilimo mbalimbali ikiwamo mpunga, lakini wanajikuta
wakiingia kwenye migogoro kutokana na kukosa
hati miliki.Mfano muwekezaji anaweza kuchukua aridhi wa mtu wakijijini na kwamba asijue nini
cha kufanya,”alisema Kihwele
MATUKIO KATIKA PICHA:
WAKAZI WA KIJIJI CHA SHISHIYU WAKIWA KATIKA KIKAO BAADA YA KUTEMBELEWA NA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA KIBINADAMU LA OXFAM TANZANIA.
AFISA ARDHI WA WILAYA YA MASWA VIVIAN MKAMBA ALIYESIMAMA AKIZUNGUMZA NA
WANAKIJIJI WA KIJIJI CHA SHISHIYU KATA YA SHISHIYU WILAYA YA MASWA
MKOANI SIMIYU.
AFISA ARDHI WA HALMASHAURI YA MASWA AKIENDELEA KUTOA ELIMU.
AFISA MAWASILIANO WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA KIBINADAMU LA OXFAM
TANZANIA KISUMA MAPUNDA AKIWAPA MAELEKEZO WANAKIJIJI WA KIJIJI CHA
SHISHIYU WILAYANI MASWA KABLA YA KUANZA KAZI YA KUREKODI MATUKIO.
KISUMA MAPUNDA AKIPITIA MOJA YA HATI MILIKI YA ARDHI ALIYOPEWA MMOJA WA WANAKIJIJI KUPITIA SHIDEPHA + NA SHIRIKA LA OXFAM
KISUMA MAPUNDA KUSHOTO AKIFANYA MAHOJIANO NA MWENYEKITI WA KAMATI YA
UKUSANYAJI PESA NA USIMAMIZI WA UPIMAJI WA ARDHI KATIKA KIJIJI CHA
SHISHIYU WILAYANI MASWA.
BAADHI YA WANA KIJIJI WAKIWA KATIKA MKUTANO HUO
KINA MAMA NAO HAWAKUWA NYUMA NAO WALIHUDHURIA KUPATA ELIMU YA HATIMILIKI YA ARDHI .
MMOJA WA WANAKIJIJI AKIWEKA SAINI KATIKA HATI YAKE MARA BAADA YA KUKABIDHIWA.
MAMA MERISIANA PETER AKIWA NA HATI YAKE YA ARDHI MARA BAADA YA KUKABIDHIWA NA AFISA ARDHI WA WILAYA YA MASWA.
AFISA WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA KIBINADAMU KUTOKA SHIRIKA LA OXFAM
TANZANIA AKIZUNGUMZA NA MWENYEKITI WA KAMATIU YA UPIMAJI WA ARDHI KIJIJI
CHA SHISHIYU KUHUSU USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA ZOEZI HILO.
KIJIJI AKIWA ANASOMA HATI YAKE YA ARDHI
MWALIMU MSTAAFU WA KIJIJI CHA SHISHIYU AKIPOKEA HATI YAKE.
MWALIMU AKISOMA HATI YAKE KWA TABASAMU KUBWA