mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Watu 7 wamefariki na wengine 26 kujeruhiwa baada ya basi la Msanga Express lililokuwa linatokea Morogoro kwenda Mahenge kugongana na basi la Luwinzo lililotokea Njombe kwenda Dar katika eneo la mbuga ya Mikumi hapo jana.
Mashuhuda
wa tukio hilo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi ambapo
dereva wa basi la Msanga alikuwa akijaribu kulipita lori, basi hilo
likagongwa upande wa kulia na kusababisha vifo vya watu sita hapo hapo
na mwingine mmoja kufariki wakati akiwa anakimbizwa kupelekwa
Hospitali.
Kamanda wa Polisi Morogoro, Leonard Paulo amesema mwili mmoja ndio uliotambulika na miili mingine 6 imehifadhiwa katika Hospitali ya St. Kizito Mikumi, madereva wa mabasi yote wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu chini ya ulinzi.
“Ilipofika
hapa mvua ilikuwa inavyesha na kulikuwa na utelezi.. kilichotokea ni
kwamba mbele kulikuwa na lori ambalo limetoroka kwenye eneo la tukio,
kwa hiyo baada ya kuliona lori alitaka kulipita kwa upande wa kulia
wakati analipita huyo mwenye basi kwa mbele ghafla kulikuwa na gari
lingine”– Kamanda wa Polisi Morogoro, Leonard Paul.
Muunguzi wa zamu Katika Hospitali ya St. Kizito, Joseph Masenga amekiri kupokea majeruhi 26 na kusema kwa sasa wanaendelea vizuri na matibabu.