mcharoman blogy fahar yako mtanzania
Shirika lisilo la kiserikali la AGPAHI limekabidhi msaada wa gari aina ya toyota land cruser kwa halmashauri mbili moja ikiwa ni halmashauri ya wilaya ya itilima pamoja na halmashauri ya wilaya ya busega kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za mapambano ya ukimwi katika halmashauri hizo.
Akikabidhi msaada huo mbele ya viongozi mbalimbali waliohudhuria katika makabiziano hayo akiwemo Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,na pia mbunge wa busega Dk Titus Kamani. Mkurugenzi mtendaji wa shirika la AGPAHI Bw;Laurean Bwanakunu amesema kuwa magari hayo yametolewa kwa ufadhili wa watu wa marekani kupitia shirika la CENTER FOR DISEASE CONTROL AND PREVENTION(CDC) la hapa nchini na pia yamegharimu shilingi Milioni 89 kila moja bila kodi.
Akitaja kazi za gari hilo Bwanakunu amesema kuwa ni pamoja na kurahisisha rufaa ya mgonjwa kutoka kituo kimoja hadi kingine,Kufanya usimamizi shirikishi vituoni,Kusambaza dawa na vitendea kazi kwenye vituo vya kutolea huduma pamoja na kurahisisha usafirishaji wa sampuli za CD4.
Mkurugenzi wa shirika la AGPAHI Ndg.Laurean Bwanakunu akitoa risala fupi katika makabiziano ya gari katika wilaya ya busega |