Watu wanaodhaniwa kuwa ni madereva wakiwa wameziba barabara ya Mwanza-Dar.
|
Madereva hao wakiendelea na mgomo.
Baadhi ya magari yaliyoathiriwa na mgomo huo.
Polisi wakiwatawanya madereva hao.
Baadhi ya magari yaliyoathiriwa na mgomo huo.
Polisi wakiwatawanya madereva hao.
MADEREVA wa daladala wilayani Misungwi, mkoani Mwanza wamefunga barabara kuu ya kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam wakitaka Serikali ya Wilaya Misungwi iwaoneshe vituo halali vya kuchukua na kushusha abiria.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa sita mchana ambapo abiria wa Misungwi hawakuweza kwenda Mwanza Mjini sababu daladala zote ziligoma kwenda na kusababisha usumbufu kwa abiria waliokuwa wakisafiri kwa muda huo.
Hata hivyo, jeshi la Polisi lilizima zoezi hilo kwa kuwatawanya watu hao kwa kuwa hawakufata taratibu za kisheria katika mgomo huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni