promotion

Alhamisi, 29 Januari 2015

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora yaanza kuchunguza tukio la KUPIGWA NA kukamatwa kwa wananchi walioshiriki mkutano wa CUF

mcharoman blogy


Untitled 1
Tume imesikitishwa na matukio yaliyotokea tarehe 27/01/2015 huko Mbagala Wilaya ya Temeke Dar-es-Salaam, matukio ambayo yameoneshwa na Kituo cha Televisheni cha “Channel Ten” ambayo yameashiria uvunjifu wa haki za binadamu.

Mnamo majira ya saa kumi na robo hadi kumi na nusu jioni, Kituo cha TV cha “Channel Ten” kilirusha picha zilizoonesha kupigwa na Polisi baadhi ya wananchi waliokamatwa kwa kile kilichoelezwa kushiriki mkutano wa Chama cha Wananchi (CUF) uliosemekana kuwa si halali.

Tume tayari imeanza kuchunguza tukio hilo na taarifa kamili itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
Bahame T. M. Nyanduga
MWENYEKITI

Hakuna maoni: