Wastani wa mshahara nchini Burkina faso ni takriban dola 150 kwa mwezi, kwa mujibu wa Mbunge kutoka baraza la mpito nchini humo ,mishahara inahusisha malipo ya vikao vya bunge, malipo ya shughuli za ofisi, malipo kwa ajili ya huduma za afya na gharama za mafuta.
Lakini Mratibu kutoka asasi moja ya kiraia ya nchini humo Herve Kam anasema malipo ya baada ya kuhudhuria bunge hayakupaswa kuwapo akieleza kuwepo kwa utofauti mkubwa kati ya Maafisa wa serikali na raia wa kawaida.
Tangu mwezi Oktoba mwaka jana Rais Blaise Compaore alipoondolewa madarakani, baraza la mpito lilikuwa na wawakilishi 90 ambao waliwakilisha lililokuwa bunge la nchi hiyo.
Mmoja wa wabunge anaunga mkono hatua hii ya kupunguza mishahara akisema hatua hii inaimarisha utawala bora na demokrasia thabiti.
Hali ilikua ya mtafaruku Baada ya kubainika kwa kiasi cha mishahara ya wabunge hali iliyosababisha ghadhabu miongoni mwa jamii kupitia kwenye mitandao wakikemea kile walichodai kutotendewa haki na kutaka viongozi kuacha kutumia madaraka yao vibaya.
Baada ya kupambana kubadilisha Serikali ya Burkinafaso, raia nchini humo wana matumaini ya kuweka mfumo mpya na mzuri wa haki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni