promotion

Jumapili, 25 Januari 2015

KIFO CHA MFALME ABDULLAH: NI UKUMBUSHO TOSHA MALI SI LOLOTE MBELE YA MUNGU!

mcharoman blogy

Aliyebebwa na kisha kulazwa hapa ni Mfalme Abdullah wa Saudia. Aliswaliwa na kuzikwa huko Riyadh mapema wiki hii.
Kuna mengi tunajifunza kwa kifo cha Mfalme huyu wa Duniani, Allah ampe kheri na jazaa huko akhera , ameen.

Mfalme ambaye alikua na utajiri usomithilika, alikua na nguvu za kusema kile nataka hiki sitaki, alikua na uwezo mkubwa, lakini yote haya ulifika muda ikawa ni mwisho wake. Mwisho wa maamuzi. Hata akivuliwa nguo alositiriwa hana uwezo wa kukemea au kujisitiri tena.

Je, umauti hauwi sababu ya sisi kurudi kwa Mola wetu? Ewe mwenye mamlaka ya ulipo, kipi kinakupa kibri na jeuri hata unamkufuru Mungu muumba wa mbingu na ardhi, alokuumba wewe tokea tone la manii?
Mfalme amezikwa na ulimwengu umeshuhudia mazishi yake yalivyokua yakawaida kabisa, kaburi lake pia ni la kawaida mno, kaburi kama ulionavyo halijajengewa na halitajengewa.


Kaburini ni wewe na Malaika wa Allah tuu. Hapo ni matendo yako mema ndio yatakayokupa unafuu sana. Jaalia wewe ndie ulielazwa pale, jee una matendo gani ya kukuepusha na adhabu za Allah. Jee uliyoyafanya juu ya mgongo wa ardhi yatakueka mbali au kukukurubisha na moto wa Jahannam?

Hakika mauti ni glasi yenye kinywaji na kila nafsi itakunywa kinywaji hicho, hakika mauti ni mawaidha, tunatakiwa tuwaidhike nayo. Hakika mauti ni mlango, na kila mtu ataupita mlango huo. Kiukweli mauti ina majina mengi sana. Na kila jina linajitosheleza nalo. Tudumisheni matendo mema ili Allah S.W atulipe mema.
ENZI Z UHAI WAKE ALIHESHIMIKA NA VIONGOZI WAKUBWA WA DUNIA




...akiwa na Rais wa Marekani, Barack Obama

...akisalimiana na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron

...akiongea na Rais wa Syria, Bashar al-Assad
Allah anatwambia...
"Mali zoote mulizonazo ni mali zangu, na Pepo ni Pepo yangu, na nyinyi ni waja wangu, enyi waja wangu, inunueni Pepo yangu kwa mali zangu"
Je, nini tupewe kama Allah anataka tuinunue Pepo yake kwa mali zake?

Hakuna maoni: